Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2025-2030 | Session 3 | Sitting 3 | Water and Irrigation | Wizara ya Maji | 16 | 2026-04-02 |
Name
Innocent Lugha Bashungwa
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Karagwe
Primary Question
MHE. INNOCENT L. BASHUNGWA aliuliza: -
Je, lini Serikali itapeleka fedha za kukamilisha ujenzi wa Mradi wa Maji wa Kayanga?
Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi Mjini
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu: -
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Maji, ninapenda kujibu swali la Mheshimiwa Innocent Lugha Bashungwa, Mbunge wa Karagwe, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inaendelea na utekelezaji wa miradi miwili ya maji katika Mji wa Kayanga Wilaya ya Karagwe Mkoani Kagera. Miradi hiyo ni pamoja na Mradi wa Miji 28 wa Rwakajunju unaotekelezwa kwa gharama ya shilingi bilioni 64.3 sambamba na mradi wa usambazaji maji katika Mji wa Kayanga unaogharimu jumla ya shilingi bilioni 1.31.
Mheshimiwa Naibu Spika, miradi hiyo kwa pamoja utekelezaji wake umefikia wastani wa 70%, ambapo inalenga kunufaisha zaidi ya wananchi 356,790 waishio kwenye Mji wa Kayanga wilayani Karagwe. Hadi kufikia mwezi Machi, 2026, Serikali imelipa jumla ya shilingi bilioni 42.98 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi hiyo.
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali itaendelea kupeleka fedha za utekelezaji wa mradi huo kulingana na hati za madai zinazowasilishwa na mkandarasi.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved