Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2025-2030 Session 3 Sitting 3 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Waziri Mkuu-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) 13 2026-04-02

Name

Hawa Subira Mwaifunga

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. HAWA S. MWAIFUNGA aliuliza: -

Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga Barabara ya kutoka Kata ya Uyui - Kakola hadi Ikomwa?

Name

Kwagilwa Reuben Nhamanilo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Handeni Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. KWAGILWA R. NHAMANILO) alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI ninapenda kujibu swali la Mheshimiwa Hawa Subira Mwaifunga, Mbunge wa Tabora Mjini, Mbunge wa Jimbo, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, Wilaya ya Tabora ina mtandao wa barabara wa jumla ya kilometa 775.64. Kati ya hizo, kilometa 61.9 ni tabaka la lami, kilometa 143.52 ni tabaka la changarawe. Barabara hii ya Uyui – Kakola – Ikomwa yenye Urefu wa kilometa 19 inaunganisha Kata tatu za Uyui - Kakola na Ikomwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwenye bajeti ya mwaka 2021/2022 barabara hii imetengewa fedha ya ukarabati. Mkandarasi wa kutekeleza kazi hii anaitwa AHAM Investment Company Limited ambapo kwa sasa yupo katika hatua za awali za kuanza kazi ambayo itadumu kwa mkataba wa miezi sita.

Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba kuwasilisha.