Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2025-2030 | Session 3 | Sitting 2 | Regional Administration and Local Government Authorities | Ofisi ya Waziri Mkuu-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) | 1 | 2026-04-01 |
Name
Kangi Alphaxard Lugola
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mwibara
Primary Question
MHE. KANGI A. LUGOLA aliuliza: -
Je, lini Serikali itakamilisha maboma 49 ya madarasa ya shule za msingi na maboma matatu ya zahanati za vijiji vitatu vya Jimbo la Mwibara?
Name
Dr. Jafar Rajab Seif
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Busanda
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. JAFAR R. SEIF) alijibu: -
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI, ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Kangi Alphaxard Lugola, Mbunge wa Jimbo la Mwibara, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha mwaka wa fedha 2022/2023 hadi kufikia 2025/2026, Serikali imetoa jumla ya shilingi milioni 379 kukamilisha maboma 33 ya madarasa na shilingi milioni 250 kukamilisha maboma matano ya zahanati za Nambaza, Muranda, Mwiseni, Neruma na Sozia katika Halmashauri ya Wilaya ya Bunda.
Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2025/2026 Serikali imetoa jumla ya shilingi milioni 241 kwa ajili ya ukamilishaji na uimarishaji wa huduma za mama na mtoto katika Zahanati ya Kabainja na shilingi milioni 50 kwa ajili ya ukamilishaji wa maboma manne ya madarasa. Serikali itaendelea kutenga bajeti kwa awamu kwa ajili ya ukamilishaji wa maboma ya madarasa na zahanati katika Halmashauri ya Wilaya ya Bunda.
Mheshimiwa Spika, ninaomba kuwasilisha.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved