Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 53 Water and Irrigation Wizara ya Ujenzi 687 2025-06-25

Name

Japhet Ngailonga Hasunga (CPA)

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Vwawa

Primary Question

MHE. JAPHET N. HASUNGA aliuliza: -

Je, lini Serikali itaanza kusambaza maji katika Vijiji vya Hatete, Ihowa, Welu II, Ruanda na Myovizi – Vwawa?

Name

Kundo Andrea Mathew

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bariadi Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inaendelea na utekelezaji wa Mradi wa Maji Hatete - Ruanda uliopo Wilaya ya Mbozi Mkoani Songwe. Kazi zinazotekelezwa katika mradi huo ni pamoja na ujenzi wa tanki la maji lenye ujazo wa lita 200,000, ujenzi wa dakio (intake), ulazaji wa mabomba umbali wa kilometa 25 sanjari na ujenzi wa vituo 10 vya kuchotea maji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, utekelezaji wa mradi huo umefikia wastani wa 55% na unatarajiwa kukamilika mwezi Disemba, 2025 na kunufaisha wananchi 6,628 waishio kwenye vijiji vitano vya Hatete, Ruanda, Ihowa, Myovizi na Welu II.