Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2020-2025 | Session 19 | Sitting 53 | Works, Transport and Communication | Wizara ya Ujenzi | 685 | 2025-06-25 |
Name
Festo Richard Sanga
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Makete
Primary Question
MHE. FESTO R. SANGA aliuliza: -
Je, lini ujenzi wa Barabara ya Usalimwani - Ikuwo hadi Nkenja kwa kiwango cha changarawe utaanza?
Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, Barabara ya Usalimwani – Ikuwo – Nkenja yenye urefu wa klometa 42.7 ni barabara ya Wilaya iliyokasimiwa kwa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) mwaka 2023. Ujenzi wa barabara hii kwa kiwango cha changarawe unatekelezwa kwa awamu kulingana na upatikanaji wa fedha.
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka wa fedha 2023/2024 na 2024/2025 jumla ya shilingi milioni 865.14 zimetumika kufanya matengenezo ya barabara hii ikiwa ni pamoja na kuongeza upana wa barabara, kuweka changarawe, kujenga makalavati pamoja na kuweka zege katika maeneo korofi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, aidha, katika mwaka wa fedha wa 2025/2026 jumla ya shilingi milioni 488.8 zimetengwa kwa ajili ya kuendelea na matengenezo ya barabara hiyo, ikiwa ni pamoja na kuweka changarawe.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved