Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 53 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 677 2025-06-25

Name

Vita Rashid Kawawa

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Namtumbo

Primary Question

MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI K.n.y. MHE. VITA R. KAWAWA aliuliza:-

Je, lini Serikali itatenga bajeti ya ujenzi wa barabara za lami katika mitaa ya Namtumbo?

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA) alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inafahamu hitaji la barabara za lami katika Mji wa Namtumbo ambazo ni takribani kilomita 28.1, na imekuwa ikitenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa barabara hizo kwa awamu, ambapo katika mwaka 2023/2024 kiasi cha shilingi milioni 890 kilitumika kujenga kilomita 1.6 za tabaka la lami.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwaka 2024/2025, Serikali ilijenga barabara yenye urefu wa kilomita 0.5 kwa tabaka la lami kwa gharama ya shilingi milioni 295. Katika mwaka 2025/2026, Serikali imeweka katika mipango yake na bajeti ujenzi wa barabara kwa tabaka la lami yenye urefu wa kilomita moja kwa shilingi milioni 475.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali itaendelea kutenga fedha kwa ajili ya kujenga barabara kwa tabaka la lami katika Mji wa Namtumbo na Makao Makuu ya Miji ya Wilaya zote hapa nchini kulingana na upatikanaji wa fedha.