Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2020-2025 | Session 19 | Sitting 49 | Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives | Wizara ya Kilimo | 633 | 2025-06-19 |
Name
Zuena Athumani Bushiri
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. FESTO R. SANGA K.n.y. MHE. ZUENA A. BUSHIRI aliuliza:-
Je, lini skimu ya umwagiliaji itajengwa katika Kata ya Arusha Chini Moshi Vijijini?
Name
Hussein Mohamed Bashe
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Nzega Mjini
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI K.n.y. WAZIRI WA KILIMO alijibu: -
Mheshimiwa Naibu Spika, katika mwaka 2024/2025 Serikali kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji inaendelea na upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa skimu mbalimbali nchini, ikiwemo Skimu ya Umwagiliaji ya Chemiko yenye ukubwa wa hekta 2,000 iliyopo katika Kata ya Arusha Chini Moshi Vijijini.
Mheshimiwa Naibu Spika, aidha, Wizara kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji katika mwaka 2025/2026 itakamilisha usanifu wa skimu hiyo na kuanza taratibu za manunuzi ili kumpata mkandarasi kwa ajili ya ujenzi. Kukamilika kwa ujenzi wa skimu hiyo, kutaongeza tija na uzalishaji wa mazao ya chakula nchini na hivyo kuwanufaisha wakulima wa Kata ya Arusha Chini.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved