Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 49 Works, Transport and Communication Wizara ya Ujenzi 630 2025-06-19

Name

Oran Manase Njeza

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mbeya Vijijini

Primary Question

MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na majibu mazuri ya Serikali, je, Serikali inaonaje umuhimu wa kuchukua mikopo kwenye taasisi mbalimbali ili waweze kuwafungia wananchi ambao hawana uwezo wa kulipa kwa mkupuo mmoja shilingi 320,000.00 mpaka 350,000.00, halafu baadaye wakaweka kwenye gharama za kutoa umeme kwa hawa wateja wakawa wanalipa kidogo kidogo? Je, Serikali inasemaje kuhusu hoja hiyo. (Makofi)

Name

Abdallah Hamis Ulega

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mkuranga

Answer

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII K.n.y. WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Naibu Spika, katika kuhakikisha kwamba Serikali inaunganisha umeme kwa wananchi wengi, jitihada mbalimbali zimechukuliwa na Serikali kuhakikisha kwamba jambo hili linafanyika vizuri.

Mheshimiwa Naibu Spika, kama Waheshimiwa Wabunge wanavyofahamu, tumepiga hatua kubwa ya kuhakikisha kwamba vijiji vyote nchini vimeweza kuunganishwa na umeme, na sasa tunakwenda kwenye eneo la vitongoji.

Mheshimiwa Naibu Spika, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba maarifa yoyote yatakayotuwezesha kuhakikisha kwamba tunawaunganisha wananchi wetu kwa ukubwa na kwa ukamilifu, Serikali itayaangalia kuona uwezekano wake wa kutekeleza na pale inapoonekana inawezekana, tutafanya hivyo. (Makofi)