Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 41 Industries and Trade Wizara ya Viwanda na Biashara 531 2025-06-06

Name

Tamima Haji Abass

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. TAMIMA HAJI ABASS aliuliza: -

Je, Serikali ina mkakati gani wa kutoa elimu kwa wajasiriamali wadogo ili kuwawezesha kuwa na vifungashio bora vya bidhaa zao? (Makofi)

Name

Exaud Silaoneka Kigahe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mufindi Kaskazini

Answer

NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru, Serikali kupitia Shirika la Maendeleo ya Viwanda (SIDO) inatekeleza mkakati wa mafunzo ya ufungashaji wa bidhaa kwa wajasiriamali ikiwemo namna ya kutengeneza vifungashio, kutumia chapa (brand) na label. Vilevile SIDO inatoa elimu kwa waundaji (designers) na wachapaji wa label za bidhaa ili kuwaongezea ujuzi katika kuwahudumia wajasiriamali. Lengo la mafunzo hayo ni kuboresha vifungashio vya bidhaa za wajasiriamali ili ziweze kushindana sokoni.

Mheshimiwa Mwenyekiti, aidha, SIDO hununua vifungashio kwa jumla (bulk procurement) kutoka nje ya nchi na kuviuza kwa rejareja na kwa bei nafuu katika Ofisi za SIDO za Mikoa kwa wajasiriamali. Hatua hiyo huwawezesha wajasiriamali kupata vifungashio bora na kwa bei nafuu, nakushukuru.