Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2020-2025 | Session 19 | Sitting 41 | Information, Culture, Arts and Sports | Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo | 527 | 2025-06-06 |
Name
Dr. Angeline Sylvester Lubala Mabula
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Ilemela
Primary Question
MHE. DKT. ANGELINE S. L. MABULA aliuliza: -
Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa kiwanja cha michezo (centre of excellence) Manispaa ya Ilemela chenye hekari 16.75 ambacho kina hati tayari?
Name
Hamis Mohamed Mwinjuma
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Muheza
Answer
NAIBU WAZIRI WA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO alijibu: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali ina dhamira ya dhati ya kuendeleza eneo hilo. Hata hivyo kwa sasa Serikali imeweka kipaumbele katika kukamilisha miradi ya ujenzi wa miundombinu ya michezo ambayo itatumika kuendeshea mashindano ya CHAN 2025 na AFCON 2027. Aidha, Serikali imeanza ujenzi wa akademia ya michezo katika Chuo cha Maendeleo ya Michezo Malya kilichopo Wilaya ya Kwimba, mkoani Mwanza ambapo utekelezaji wa mradi huo umefikia asilimia 25.4. Hivyo kwa kuanzia, wananchi wa Mkoa wa Mwanza watanufaika na mradi huo mara utakapokamilika, huku tukiendelea kujipanga na utekelezaji wa mradi katika Manispaa ya Ilemela.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved