Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 41 Lands, Housing and Human Settlement Development Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi 526 2025-06-06

Name

Dr. Christine Gabriel Ishengoma

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA aliuliza: -

Je, Serikali ina mkakati gani wa kumaliza migogoro ya wafugaji na wakulima Mkoani Morogoro?

Name

Geophrey Mizengo Pinda

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kavuu

Answer

NAIBU WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inatambua kuwepo kwa migogoro ya wafugaji na wakulima Mkoani Morogoro. Hata hivyo, Serikali inaendelea kuchukua hatua mbalimbali kukabiliana na migogoro hiyo ambapo baadhi ya hatua hizo ni pamoja na kuweka mipango ya matumizi bora ya ardhi za vijiji ili kubainisha maeneo ya kilimo sambamba na maeneo ya wafugaji kupitia Tume ya Taifa ya Matumizi Bora ya Ardhi. Aidha, hatua nyingine ni kupitia Mradi wa KKK ambapo miji chipukizi kama ilivyo kwa miji ya halmashauri kupangwa, kupimwa na kumilikishwa sambamba na kuweka mipango ya matumizi bora ya ardhi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nitoe rai kwa wananchi kuhakikisha kuwa wanatumia ardhi kuendana na mipango ya matumizi iliyopangwa ili kuondoa muingiliano wa matumizi ya ardhi ambayo imekuwa ni chanzo cha migogoro ya wakulima na wafugaji.