Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2020-2025 | Session 19 | Sitting 41 | Water and Irrigation | Wizara ya Maji | 525 | 2025-06-06 |
Name
Tarimba Gulam Abbas
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kinondoni
Primary Question
MHE. TARIMBA G. ABBAS aliuliza: -
Je, nini kauli ya Serikali juu ya changamoto ya maji maeneo ya Jimbo la Kinondoni hususani Kata za Mwananyamala na Makumbusho?
Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi Mjini
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru, dhamira ya Serikali ni kuhakikisha maeneo yote ya Jiji la Dar es Salaam yanapata huduma ya majisafi, salama na yenye kutosheleza, zikiwemo Kata za Mwananyamala na Makumbusho. Kata hizo zimekuwa na ongezeko kubwa la watu huku miundombinu yake ya maji ikiwa ni ya muda mrefu na inakabiliwa na changamoto ya uchakavu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kukabiliana na changamoto hiyo, Serikali katika mwaka wa fedha 2025/2026 itakarabati miundombinu ya maji katika eneo la Kisiwani Msikitini, kwa ajili ya kuboresha upatikanaji wa huduma ya maji katika maeneo yote ya Kata za Mwananyamala na Makumbusho, ahsante sana.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved