Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2020-2025 | Session 19 | Sitting 49 | Regional Administration and Local Government Authorities | Ofisi ya Rais TAMISEMI. | 627 | 2025-06-19 |
Name
Agnesta Lambert Kaiza
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. ESTHER N. MATIKO K.n.y. MHE. AGNESTA L. KAIZA aliuliza:-
Je, ni maeneo gani ya kuweka mkazo ili Sekta nyingine zitekeleze na kuwa sehemu ya utekelezaji wa azma ya Ugatuzi wa Madaraka?
Name
Zainab Athuman Katimba
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA) alijibu: -
Mheshimiwa Naibu Spika, dhana ya Ugatuzi wa Madaraka nchini inasimamiwa kupitia Andiko la Kisera la Maboresho ya Serikali za Mitaa la Mwaka 1998 (Policy Paper on Local Government Reform, 1998) na imelenga kupeleka madaraka, rasilimali na maamuzi kutoka Serikali Kuu kwenda Serikali za Mitaa.
Mheshimiwa Naibu Spika, faida mbalimbali zimepatikana kwa kutekeleza sera hii ikiwa ni pamoja na kuimarika kwa ushiriki wa wananchi katika kupanga, kusimamia na kutathmini maendeleo ya maeneo na kuimarisha utoaji wa huduma za kijamii kwa umma, mathalan elimu na afya katika mamlaka za Serikali za Mitaa.
Mheshimiwa Naibu Spika, ili kuharakisha suala la ugatuzi, Serikali imeandaa Rasimu ya Sera kamili ya Taifa ya Ugatuzi ambayo imeshaanza kujadiliwa katika ngazi mbalimbali za maamuzi, na pindi itakapokamilika na kuanza kutumika itaongeza ufanisi na kuimarisha ugatuzi katika sekta mbalimbali Serikalini.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved