Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 41 Union Affairs Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano 522 2025-06-06

Name

Zahor Mohamed Haji

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mwera

Primary Question

MHE. ZAHOR MOHAMMED HAJI aliuliza: -

Je, ni lini Serikali italeta muswada wa sheria kuhusu changamoto za Muungano zilizopatiwa ufumbuzi ili sasa ziwe kwa mujibu wa sheria?

Name

Khamis Hamza Khamis

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Uzini

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MUUNGANO NA MAZINGIRA alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakubaliana na Mheshimiwa Mbunge kuwa mpaka sasa jumla ya changamoto 22 za Muungano zimekwishapatiwa ufumbuzi. Aidha, katika Kikao cha Kamati ya Pamoja ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SJMT) na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) ambacho kilifanyika tarehe 4 Aprili, 2025 Ikulu Dar es Salaam kwa ajili ya kutafuta ufumbuzi wa changamoto za Muungano, kilitoa maelekezo kwa Ofisi za Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kulifanyia kazi jambo hilo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, aidha, mara baada ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa taarifa hiyo, itatolewa kwa umma, ninakushukru.