Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2020-2025 | Session 19 | Sitting 37 | Natural Resources and Tourism | Wizara ya Maliasili na Utalii | 482 | 2025-06-02 |
Name
Miraji Jumanne Mtaturu
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Singida Mashariki
Primary Question
MHE. MIRAJI J. MTATURU aliuliza: -
Je, Serikali ina mpango gani wa kuondoa tembo ambao wanasumbua na kuharibu mashamba ya wananchi wa Singida Mashariki?
Name
Dunstan Luka Kitandula
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mkinga
Answer
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII alijibu: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kudhibiti tembo wanaovamia na kuharibu mashamba ya wananchi wa Singida Mashariki, Serikali kupitia TAWA inaendelea kuchukua hatua mbalimbali ikiwemo kuweka vikosi viwili vyenye Askari 24 wakiwemo Wahifadhi 13 na Askari Wanyamapori wa Vijiji 11 na kutoa magari matatu. Vilevile, kuimarisha matumizi ya ndegenyuki kwa kuwafukuza tembo kutoka kwenye maeneo ya wananchi na kuwarejesha hifadhini.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mathalani, kati ya mwezi Novemba, 2024 na Mei, 2025 kikosi maalum cha Askari wa Hifadhi 18 na VGS Sita, kikitumia ndege nyuki mbili na mabomu baridi kiliweka kambi katika Jimbo la Singida Mashariki, Wilayani Ikungi na kufanikiwa kudhibiti makundi 23 ya tembo kwa kuwarudisha ndani ya hifadhi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inaendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu namna ya kuepuka madhara yanayoweza kusababishwa na wanyamapori wakali na waharibifu wakiwemo tembo. Mathalani, kwa kipindi cha Julai, 2024 hadi Mei, 2025, elimu hiyo imetolewa kwa wananchi 517 na Askari 110 wa Jeshi la Akiba katika Kata za Mkiwa, Igombwe, Iglansonia, Mang’onyi, Issuna, Ntuntu na Ikungi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, aidha, Serikali itaendelea kutumia teknolojia ikiwemo ndegenyuki na kufunga visukuma mawimbi ili kufuatilia mienendo ya tembo na kuwadhibiti.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved