Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 37 Works and Transport Wizara ya Ujenzi 477 2025-06-02

Name

Dr. Oscar Ishengoma Kikoyo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Muleba kusini

Primary Question

MHE. DKT. OSCAR I. KIKOYO aliuliza: -

Je, kwa nini watumiaji wa Daraja la Mwalimu Julius Kambarage Nyerere wanalipia kila wanapopita huku watumiaji wa Daraja la Tanzanite hawalipi? (Makofi)

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, watumiaji wa Daraja la Mwalimu Julius Kambarage Nyerere wanalipia kila wanapopita kwa sababu daraja hili limejengwa kwa utaratibu wa ubia (Public Private Partnership - PPP) ambapo mwekezaji hurudisha fedha zake alizowekeza pamoja na faida kutokana na tozo kwa watumiaji. Kwa upande wa Daraja la Tanzanite watumiaji hawalipi kwa sababu daraja hilo limejengwa kwa utaratibu wa kawaida kama uliotumika kujenga madaraja mengine nchini.