Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 37 Enviroment Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano 476 2025-06-02

Name

Naghenjwa Livingstone Kaboyoka

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. NAGHENJWA L. KABOYOKA aliuliza: -

Je, Serikali ina mpango gani wa kuhakikisha usafi wa mazingira kwenye makazi ya watu hasa mijini?

Name

Eng. Hamad Yussuf Masauni

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kikwajuni

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, AJIRA, VIJANA, NA WENYE ULEMAVU (MHE. PASCHAL P. KATAMBI) K.n.y. WAZIRI WA NCHI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MUUNGANO NA MAZINGIRA alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Naghenjwa Livingstone Kaboyoka, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kuimarisha uhifadhi wa taka na usafi wa miji na majiji nchini, Serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais imeandaa miongozo mahususi inayoelekeza mbinu za kupunguza uzalishaji wa taka. Miongozo hii ni pamoja na Mwongozo wa Kupunguza, Kutumia Tena na Rejeleza; Mwongozo wa Uwajibikaji wa Mzalishaji wa Taka Zitokanazo na Bidhaa Anazozizalisha; na Mwongozo wa Uwekezaji katika Sekta Ndogo ya Udhibiti wa Taka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, utekelezaji wa miongozo hii umeweza kupunguza baadhi ya taka hususan taka za plastiki zitokanazo na vinywaji vinavyohifadhiwa katika chupa za plastiki. Aidha, Serikali ipo katika hatua za mwisho za kuandaa Mkakati wa Taifa wa Udhibiti wa Taka, ambapo mkakati huo utahusisha usimamizi wa taka katika mnyororo mzima wa uzalishaji na udhibiti wa taka kuanzia katika vyanzo vya uzalishaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kupitia Bunge lako Tukufu ninaomba kuhimiza Sekta Binafsi kuendelea kuwajibika kwa taka zinazotokana na bidhaa zinazozalishwa pamoja na kuchangamkia fursa ya udhibiti wa taka kwa kuwa taka ni mali na ni malighafi katika uzalishaji wa bidhaa nyingine.

Mheshimiwa Mwenyekiti, aidha, wananchi wote kujenga tabia ya usafi wa mazingira yao na kuhakikisha kuwa kila mmoja wetu anawajibika kwa taka anazozizalisha, ili kuifanya Tanzania kuwa safi na salama na kuiepusha jamii na magonjwa ya milipuko yanayoweza kutokea, ahsante.