Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 37 Finance Wizara ya Fedha 480 2025-06-02

Name

Prof. Patrick Alois Ndakidemi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Moshi Vijijini

Primary Question

MHE. PROF. PATRICK A. NDAKIDEMI aliuliza: -

Je, Serikali imejiandaa vipi kukabiliana na mabadiliko ya sera za baadhi ya nchi tajiri kulisaidia Taifa letu kukuza uchumi?

Name

Dr. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Iramba Magharibi

Answer

WAZIRI WA FEDHA alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kujibu swali kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inaendelea na jitihada mbalimbali za kuongeza mapato ya ndani ili kuhakikisha kuwa sehemu kubwa ya bajeti inagharamiwa kwa kutumia mapato ya ndani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, aidha, kwa kutambua umuhimu wa mahitaji ya kibajeti ikiwemo ugharamiaji wa miradi ya maendeleo, Serikali itaendelea kuvutia ushiriki wa sekta binafsi katika ugharamiaji wa miradi ya maendeleo kwa kutumia njia mbadala ikiwemo ubia kati ya sekta ya umma na sekta binafsi. Hii itasaidia kuipunguzia Serikali mzigo wa kukopa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo na kupunguza utegemezi wa kibajeti kutoka kwa Washirika wa Maendeleo.