Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2020-2025 | Session 19 | Sitting 45 | Health and Social Welfare | Wizara ya Afya | 584 | 2025-06-12 |
Name
Mariamu Nassoro Kisangi
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. MARIAM N. KISANGI aliuliza: -
Je, Serikali ina mpango gani wa kudhibiti ongezeko la Wagonjwa wa Kansa nchini?
Name
Dr. Godwin Oloyce Mollel
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Siha
Answer
NAIBU WAZIRI WA AFYA alijibu: -
Mheshimiwa Spika, Serikali inatekeleza mikakati mbalimbali katika kukabiliana na ongezeko la wagonjwa wa Kansa kwa kufanya yafuatayo: -
(a) Kutoa elimu kwa umma kuhusu kujikinga na ugonjwa wa saratani kupitia vipindi vya redio, televisheni, machapisho, magazeti na mitandao ya kijamii;
(b) Serikali inatoa chanjo ya Human Papilloma Virus kwa wasichana ili kuwakinga na kirusi kinachosababisha saratani ya mlango wa kizazi;
(c) Kuanzisha huduma za awali za uchunguzi na matibabu ya saratani kuanzia ngazi ya zahanati hadi hospitali za Taifa;
(d) Serikali imeimarisha huduma za kibingwa za uchunguzi na matibabu kwa kuhakikisha uwepo wa wataalamu na vifaa tiba kwa ajili ya kukabiliana na Saratani.
Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved