Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2020-2025 | Session 19 | Sitting 37 | Regional Administration and Local Government Authorities | Ofisi ya Rais TAMISEMI. | 472 | 2025-06-02 |
Name
Masache Njelu Kasaka
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Lupa
Primary Question
MHE. MASACHE N. KASAKA aliuliza: -
Je, lini Selikali itapeleka Vifaatiba na Wataalam katika Zahanati za Wilaya ya Chunya?
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imeendelea kutoa vibali vya ajira kila mwaka, ambapo katika kipindi cha mwaka wa fedha 2020/2021 hadi 2024/2025 jumla ya watumishi wa kada ya afya 34,720 wameajiriwa na kupangiwa vituo kote nchini.
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kipindi cha mwaka wa fedha 2020/2021 hadi 2024/2025 Halmashauri ya Wilaya ya Chunya imepokea jumla ya watumishi 151 wa kada ya afya na watumishi 46 wamepangiwa Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Chunya, 44 ngazi ya vituo vya afya na watumishi 61 katika zahanati.
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kuboresha upatikanaji wa vifaatiba; katika mwaka wa fedha 2024/2025, Serikali imepeleka shilingi milioni 400 kwa ajili ya ununuzi wa vifaatiba katika Halmashauri ya Wilaya ya Chunya, ambapo shilingi milioni 100 zimetumika kununua vifaatiba, ngazi ya zahanati.
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka wa fedha 2025/2026 Serikali imetenga shilingi milioni 200 kwa ajili ya ununuzi wa vifaatiba ambapo shilingi milioni 50 zitatumika kununua vifaatiba, ngazi ya zahanati, katika Halmashauri ya Chunya.
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka wa fedha 2024/2025, Serikali imepeleka shilingi milioni 400 kwa ajili ya ununuzi wa vifaatiba katika Halmashauri ya Wilaya ya Chunya ambapo shilingi milioni 100 zimetumika kununua vifaatiba ngazi ya zahanati.
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka wa fedha 2025/2026 Serikali imetenga shilingi milioni 200 kwa ajili ya ununuzi wa vifaatiba ambapo shilingi milioni 50 zitatumika kununua vifaatiba ngazi ya zahanati katika Halmashauri ya Chunya.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved