Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2020-2025 | Session 19 | Sitting 45 | Union Affairs | Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano | 578 | 2025-06-12 |
Name
Soud Mohammed Jumah
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Donge
Primary Question
MHE. SOUD MOHAMMED JUMAH aliuliza: -
Je, kuna mkakati gani kuimarisha uhifadhi wa mazingira ya Mradi wa Bwawa la Umeme la Mwalimu Nyerere ili kuhakikisha uendelevu wa Mradi huo?
Name
Khamis Hamza Khamis
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Uzini
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MUUNGANO NA MAZINGIRA alijibu: -
Mheshimiwa Spika, katika kuimarisha uhifadhi wa mazingira ikiwemo uhifadhi wa Mazingira ya Mradi wa Bwawa la Mwalimu Nyerere, Serikali imechukua hatua mbalimbali ikiwemo kuendelea kupanda na kutunza miti kwenye vyanzo vya maji, kuendelea kutoa elimu ya mazingira, kusimamia utekelezaji wa Mwongozo wa Taifa wa Matumizi endelevu ya Ardhi Eneo la Hifadhi ya Mita 60 kutoka kwenye vyanzo vya maji, pamoja na kuunda kamati za mazingira kwa ajili ya kudhibiti uharibifu wa mazingira kwenye vyanzo vya maji.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved