Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 33 Industries and Trade Wizara ya Viwanda na Biashara 424 2025-05-27

Name

Kavejuru Eliadory Felix

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Buhigwe

Primary Question

MHE. KAVEJURU E. FELIX aliuliza: -

Je, Serikali ina mpango gani wa kufanya Mkoa wa Kigoma kuwa lango la biashara?

Name

Exaud Silaoneka Kigahe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mufindi Kaskazini

Answer

NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inaendelea kutekeleza mkakati wa kuifanya Kigoma kuwa lango la biashara ikiwa ni pamoja na kuimarisha biashara za mpakani ikiwemo Bandari ya Kigoma/Kibirizi katika kusafirisha bidhaa na abiria kwenda katika miji ya Momba na Kalemie nchini DRC pamoja na mipaka ya Manyovu na Mabamba katika Halmashauri za Wilaya ya Buhigwe na Kibondo ambayo inatumika na wafanyabiashara wengi kupitisha mizigo kwenda nchini Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Mheshimiwa Naibu Spika, aidha, Serikali imeendelea kuifungua Kigoma kuwa kitovu cha Biashara na Uwekezaji kwa kutumia fursa ya kijiografia kwa kuboresha miundombinu ya Barabara, Umeme, Afya, Elimu, Uwanja wa Ndege na Ajira, mfano barabara ya kutoka Kigoma kwenda Tabora.