Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 33 Public Service Management Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora) 423 2025-05-27

Name

Maimuna Salum Mtanda

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Newala Vijijini

Primary Question

MHE. MAIMUNA S. MTANDA aliuliza:-

Je, Serikali ina mpango gani wa kukabiliana na upungufu wa watumishi hususan Walimu na Watoa Huduma za Afya - Newala Vijijini?

Name

Deus Clement Sangu

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kwela

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa mwaka wa fedha 2023/2024 Serikali iliidhinisha kibali na kuajiri Walimu 12,015 na watoa huduma za afya 13,625. Kati ya nafasi hizo walimu 30 na Watoa Huduma za Afya nafasi 42 waliajiriwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Newala ili kukabiliana na upungufu wa watumishi katika sekta hizo.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inaendelea kukabiliana na upungufu huo ambapo katika mwaka wa fedha 2024/2025, Serikali imepanga kuajiri jumla ya walimu 10,652 na watoa huduma za afya 10,449 ambapo kati ya nafasi hizo, walimu wapya 49 na watoa huduma za afya nafasi 52 watapangiwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Newala.