Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2020-2025 | Session 19 | Sitting 33 | Regional Administration and Local Government Authorities | Ofisi ya Rais TAMISEMI. | 421 | 2025-05-27 |
Name
Boniphace Mwita Getere
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bunda
Primary Question
MHE. BONIPHACE M. GETERE aliuliza:-
Je, kwa nini vijiji vyenye maeneo ya mnada havipati mgao wa 20% ya mapato ya mnada?
Name
Zainab Athuman Katimba
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA) alijibu:-
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inatambua umuhimu wa vijiji vinavyotoa maeneo kwa ajili ya shughuli za minada na mchango wake katika ukusanyaji wa mapato ya ndani ya Halmashauri.
Mheshimiwa Naibu Spika, mapato yanayokusanywa kutoka kwenye minada huingizwa katika mfuko mkuu wa Halmashauri na kutumika kwa mujibu wa bajeti iliyoidhinishwa kwa kuzingatia vipaumbele vya maendeleo katika maeneo yote ya Halmashauri, ikiwemo vijiji vinavyohusika na minada. Vilevile, halmashauri zote nchini zina wajibu wa kuchangia kwenye miradi ya maendeleo kati ya 20% hadi 70% ya mapato ya ndani kulingana na daraja la Halmashauri.
Mheshimiwa Naibu Spika, ili kuwezesha vijiji kugharamia shughuli ndogo ndogo za kiofisi Serikali imetoa maelekezo katika Mwongozo wa Bajeti kwa kila halmashauri kupeleka kati ya shilingi 100,000 hadi shilingi 200,000 kwenye vijiji kila robo mwaka kutoka kwenye mapato ya ndani kwa ajili ya uendeshaji wa ofisi. Kiasi hicho cha fedha, hutegemea daraja la halmashauri husika.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved