Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2020-2025 | Session 19 | Sitting 33 | Regional Administration and Local Government Authorities | Ofisi ya Rais TAMISEMI. | 419 | 2025-05-27 |
Name
Dr. Medard Matogolo Kalemani
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Chato
Primary Question
MHE. DKT. MEDARD M. KALEMANI aliuliza: -
Je, lini Serikali itakamilisha ujenzi wa vituo vya afya Kata za Nyamilembe, Kasenga na Ilyamachele vilivyoanza kujengwa kwa nguvu za Wananchi?
Name
Zainab Athuman Katimba
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA) alijibu:-
Mheshimiwa Naibu Spika, mwaka 2024/2025, Serikali imetoa shilingi milioni 250 kwa ajili ya ujenzi wa jengo la kuhudumia wagonjwa wa nje OPD katika Kituo cha Afya Kasenga.
Mheshimiwa Naibu Spika, Kituo cha Afya Kata ya Nyamilembe kipo kwenye Mpango wa kupokea fedha kutoka Mfuko wa TASAF katika mwaka 2024/2025, ambapo tayari Halmashauri ya Wilaya ya Chato imewasilisha maombi makao makuu.
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali itaendelea kutenga fedha kwa awamu kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa vituo vya afya vilivyoanza ujenzi kwa nguvu za wananchi katika Kata za Kimkakati kote nchini zikiwemo Kata za Nyamilembe, Kasenga na Ilyamchele katika Halmashauri ya Chato.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved