Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2020-2025 | Session 19 | Sitting 33 | Regional Administration and Local Government Authorities | Ofisi ya Rais TAMISEMI. | 418 | 2025-05-27 |
Name
Francis Isack Mtinga
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Iramba Mashariki
Primary Question
MHE. FRANCIS I. MTINGA aliuliza: -
Je, lini Serikali itatekeleza ahadi ya ukarabati wa Vituo vya Afya Mkalama na Kinyangiri ambavyo ni chakavu?
Name
Zainab Athuman Katimba
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA) alijibu: -
Mheshimiwa Naibu Spika, Vituo vya Afya vya Mkalama na Kinyangiri ni miongoni mwa vituo vya afya kongwe 203 ambavyo Serikali imeviainisha kwa ajili ya ukarabati na kuongeza miundombinu yake.
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inakamilisha ukarabati wa hospitali 50 kongwe nchini na baadaye itafanya ukarabati wa vituo vya afya na zahanati kongwe kote nchini vikiwemo vituo vya afya vya Mkalama na Kinyangiri.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved