Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 33 Youth, Disabled, Labor and Employment Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu 417 2025-05-27

Name

Salim Mussa Omar

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Gando

Primary Question

MHE. SALIM MUSSA OMAR aliuliza: -

Je, Serikali haioni haja ya kutengeneza Kanuni zitakazoweka kima cha chini cha mishahara ya Wafanyakazi wa Majumbani?

Name

Paschal Katambi Patrobas

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Shinyanga Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU (MHE. PASCHAL P. KATAMBI) alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Salim Mussa Omar, Mbunge wa Gando kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inatambua umuhimu wa wafanyakazi wa nyumbani na hivyo imeendelea kuweka kanuni tajwa mwaka 2022. Kupitia Tangazo la Kima cha Chini cha Mshahara Na. 687, Serikali iliweka kima cha chini cha mshahara kwa sekta binafsi ikiwemo sekta ya wafanyakazi wa nyumbani.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa mujibu wa sheria, tangazo hili linadumu kwa miaka mitatu, na hivyo kwa sasa Serikali kupitia Bodi ya Kima cha Chini cha Mshahara kwa Sekta Binafsi inaendelea kukamilisha utafiti wa kima kipya cha chini cha mshahara ambacho pia kitajumuisha sekta ya wafanyakazi wa nyumbani. Ahsante.