Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2020-2025 | Session 19 | Sitting 29 | Information, Communication and Information Technology | Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari | 377 | 2025-05-21 |
Name
Festo Richard Sanga
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Makete
Primary Question
MHE. FESTO R. SANGA aliuliza: -
Je, lini Serikali itafikia makubaliano na kampuni zinazotoa huduma ya Internet kwa Satellite duniani kutoa huduma hapa nchini?
Name
Maryprisca Winfred Mahundi
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI alijibu: -
Mheshimiwa Naibu Spika, ili kutoa huduma ya intaneti hapa nchini kwa kutumia satellite, kampuni inahitaji kuwa na leseni ya kutoa huduma hiyo kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA). Hadi sasa, TCRA imetoa leseni kwa mtoa huduma mmoja wa satellite (Connect Broadband Tanzania Limited) ambaye alipewa leseni mwaka 2021 baada ya kukikidhi vigezo vyote vinavyohitajika kwa mujibu wa sheria.
Mheshimiwa Naibu Spika, maombi ya watoa huduma wote yamekuwa yanashughulikiwa kwa mujibu wa Sheria na Kanuni, na pindi yanapokidhi vigezo wanapewa leseni. Aidha, utaratibu mzima wa upatikanaji wa leseni, aina ya leseni pamoja na masharti ya leseni vyote hivyo vinapatikana katika tovuti (website) ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).
Mheshimiwa Naibu Spika, TCRA inakaribisha na inaendelea kupokea maombi kutoka kwa Kampuni mbalimbali zenye sifa ya kutoa huduma za satellite kwa mujibu wa Sheria na Kanuni zinazosimamia sekta ya mawasiliano hapa Nchini.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved