Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 29 Industries and Trade Wizara ya Viwanda na Biashara 375 2025-05-21

Name

Constantine John Kanyasu

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Geita Mjini

Primary Question

MHE. HUSSEIN N. AMAR K.n.y. MHE. CONSTANTINE J. KANYASU aliuliza: -

Je, Serikali haioni haja ya kukifufua Kiwanda cha Pamba na Mafuta Kasamwa kwa kuwa hivi karibuni nchi ilikabiliwa na uhaba wa mafuta?

Name

Exaud Silaoneka Kigahe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mufindi Kaskazini

Answer

NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, ninakushukuru. Serikali kupitia Bodi ya Pamba (TCB) mwaka 2020 ilifanya tathmini juu ya hali ya viwanda vya kuchambua pamba nchini.

Mheshimiwa Naibu Spika, tathmini hiyo iliwezesha Chama cha Ushirika Geita kufanya maamuzi ya kufufua Kiwanda cha Kuchambua Pamba cha Kasamwa kupitia mkutano wa tarehe 27 Machi, 2025 kwa kukopa fedha katika Benki ya Azania, mkopo wa kiasi cha shilingi bilioni 8.68. Aidha, chama kimepanga kuanza na kiwanda cha kuchambua pamba na kiwanda cha kukamua mafuta kitafuata baada ya hapo.