Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2020-2025 | Session 19 | Sitting 29 | Water and Irrigation | Wizara ya Maji | 368 | 2025-05-21 |
Name
Mrisho Mashaka Gambo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Arusha Mjini
Primary Question
MHE. MRISHO M. GAMBO aliuliza: -
Je, lini Serikali itakamilisha mfumo wa maji taka Kiwanda cha A - Z ili kuondoa changamoto ya Wananchi wa Kata ya Olmot – Arusha?
Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi Mjini
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu: -
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inaendelea na utekelezaji wa Mradi wa Ujenzi wa Miundombinu ya Uondoshaji Majitaka wa Olmoti utakaonufaisha Kiwanda cha A to Z pamoja na wakazi zaidi ya 1,200 wa Kata ya Olmot – Arusha. Kazi zinazotekelezwa katika mradi huo ni pamoja na ulazaji wa mabomba umbali wa kilometa 9.206, ujenzi wa nguzo 15 za kushikilia bomba kwenye vivuko pamoja na ujenzi wa Chemba 188 za ukaguzi wa mfumo wa majitaka. Hadi sasa utekelezaji wa mradi huo umefikia wastani wa 78% na unatarajiwa kukamilika mwezi Juni, 2025.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved