Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 29 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 366 2025-05-21

Name

Omari Mohamed Kigua

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kilindi

Primary Question

MHE. OMARI M. KIGUA aliuliza: -

Je, lini Serikali itajenga daraja linalounganisha Kijiji cha Negero – Kilindi?

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA) alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inatambua umuhimu wa daraja linalounganisha Kijiji cha Negero – Kilindi katika kuchochea shughuli za kiuchumi katika eneo hilo. Katika mwaka 2023/2024, Serikali ilitumia shilingi milioni 70 kufanya usanifu wa Daraja la Mto Negero ili kupata gharama halisi za ujenzi wa daraja hilo. Usanifu ulikamilika mwezi Machi, 2025.

Mheshimiwa Naibu Spika, kazi inayoendelea sasa ni kupitia taarifa ya usanifu na baada ya kukamilika na kupata gharama halisi, daraja hili litaombewa fedha kwa ajili ya kuanza ujenzi.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa sasa wananchi wa eneo hilo wanatumia kivuko cha chuma cha waenda kwa miguu (Pedestrian Suspension Bridge) chenye upana wa mita 100 kilichojengwa na kukamilika Desemba, 2021 kwa gharama ya shilingi milioni 66.68 ili kuwapunguzia adha katika eneo hilo.