Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 29 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 364 2025-05-21

Name

Timotheo Paul Mnzava

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Korogwe Vijijini

Primary Question

MHE. RASHID A. SHANGAZI K.n.y. MHE. TIMOTHEO P. MNZAVA aliuliza: -

Je, lini Serikali itaanzisha Vijiji vipya kwenye maeneo ya Songea, Mkamani, Kwaluma Masimba na Sekioga – Korogwe Vijijini?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, uanzishaji wa maeneo ya utawala hutekelezwa kwa mujibu wa Sheria za Serikali za Mitaa Sura ya 287 na 288 pamoja na Mwongozo wa uanzishwaji wa maeneo ya utawala wa Mwaka 2014 ambao umeainisha utaratibu na vigezo vinavyopaswa kufuatwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, miongozo na vigezo vya kuanzisha kijiji kipya kwa mujibu wa Mwongozo wa Uanzishaji wa Mamlaka za Serikali za Mitaa wa Mwaka 2014 ni idadi ya watu wasiopungua 5,000. Katika kijiji kipya na kijiji kinachobaki kinapaswa kuwa na watu 10,000, hivyo kufanya jumla ya watu 15,000. Kwa mujibu wa takwimu za sensa ya watu na makazi iliyofanyika mwaka 2022 vijiji vya Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe vina idadi pungufu ya watu 15,000.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imetoa kipaumbele katika kuboresha na kukamilisha miundombinu ya msingi kwenye maeneo yaliyoanzishwa ili yaweze kutoa huduma kwa jamii na baadaye kuendelea na maeneo mengine kwa kufuata taratibu na vigezo vilivyoainishwa, ahsante.