Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 46 Industries and Trade Wizara ya Viwanda na Biashara 592 2025-06-16

Name

Janeth Elias Mahawanga

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. JANETH E. MAHAWANGA aliuliza: -

Je, Serikali ina Sera za kuwawezesha wanawake wajasiriamali kutumia teknolojia ya habari kuongeza ufanisi wa biashara zao?

Name

Dr. Selemani Said Jafo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kisarawe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU (MHE. PASCHAL P. KATAMBI) K.n.y. WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA alijibu: -

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Viwanda na Biashara, ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Janeth Elias Mahawanga, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia mamlaka zake ina sera mbalimbali za kuwawezesha wananchi wakiwemo wajasiliamali wanawake kutumia teknolojia ya habari ili kuongeza ufanisi wa shughuli zao ikiwemo biashara. Sera hizo ni pamoja na Sera ya Taifa ya Biashara ya Mwaka 2003 Toleo la 2023, Sera ya Taifa ya Posta ya Mwaka 2003, Sera ya Taifa ya Mawasiliano ya Mwaka 1997 na Sera ya Taifa ya TEHAMA ya Mwaka 2016 ambazo zinatambua Biashara Mtandao inayowezeshwa na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano.

Mheshimiwa Spika, aidha, kwa kutambua uwepo wa changamoto za Teknolojia ya Habari katika kufanya biashara, Serikali imeandaa Mkakati wa Kitaifa wa Biashara Mtandao (National Electronic Commerce Strategy) ili kuwawezesha wajasiriamali wakiwemo wanawake kufanya biashara mtandaoni. Ninakushukuru.