Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 46 Finance Wizara ya Fedha 591 2025-06-16

Name

Mohammed Said Issa

Sex

Male

Party

ACT

Constituent

Konde

Primary Question

MHE. MOHAMED SAID ISSA aliuliza: -

Je, changamoto zipi zinazorotesha ukusanyaji wa mapato katika mfumo mpya wa kuchakata Kodi ya Forodha ambao ni "single window"?

Name

Hamad Hassan Chande

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kojani

Answer

NAIBU WAZIRI WA FEDHA alijibu: -

Mheshimiwa Spika, ahsante sana, single window ni dirisha moja la kufanikisha uwasilishaji wa nyaraka mbalimbali kutoka kwa wadau wote muhimu katika mnyororo wa ugomboaji mizigo ya forodha.

Mheshimiwa Spika, itakumbukwa kuwa kabla ya Mfumo wa Single Window, mteja alilazimika kuwasilisha nyaraka na vielelezo mbalimbali kwenda kila idara ya Serikali inayohusika katika mnyororo wa ugomboaji wa mizigo, na hivyo kusababisha usumbufu mkubwa na kuchelewesha ugomboaji wa mizigo forodhani.

Mheshimiwa Spika, ninapenda kutoa hofu kuwa single window haitaweza kupelekea uzoroteshaji wa ukusanyaji mapato ya Serikali bali utasaidia kuondoa usumbufu kwa wateja na kurahisisha ukokotoaji wa kodi mbalimbali kupitia Mfumo wa TANCIS uliohuishwa.