Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2020-2025 | Session 19 | Sitting 46 | Regional Administration and Local Government Authorities | Ofisi ya Rais TAMISEMI. | 587 | 2025-06-16 |
Name
Toufiq Salim Turky
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mpendae
Primary Question
MHE. SHALLY J. RAYMOND K.n.y. MHE. TOUFIQ SALIM TURKY aliuliza: -
Je, Serikali imejipangaje kutatua changamoto ya ucheleweshwaji wa kupandisha hadhi vituo vya afya na zahanati zinazookoa maisha ya wananchi nchini?
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu: -
Mheshimiwa Spika, utaratibu wa kupandisha hadhi kituo cha kutolea huduma kutoka ngazi ya chini kwenda ngazi ya juu unazingatia miongozo na vigezo mbalimbali vya ngazi husika ya kituo. Miongoni mwa vigezo hivyo ni pamoja na uwepo wa eneo toshelezi kwa ngazi ya kituo, miundombinu, vifaatiba na watumishi.
Mheshimiwa Spika, katika kuharakisha taratibu za usajili na kupandisha hadhi vituo vya kutolea huduma za afya, Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais, TAMISEMI imeboresha utaratibu kwa kuanzisha mfumo wa kuwasilisha maombi kwa njia ya mtandao kutoka ngazi ya msingi hadi ngazi ya Wizara (Health Facility Registration System).
Mheshimiwa Spika, mfumo huu umewezesha kupunguza mlolongo wa kuwasilisha na kujibiwa kwa maombi ya usajili na upandishaji hadhi wa vituo vya afya kutoka siku 60 hapo awali hadi siku saba ikiwa kituo kinachopandishwa hadhi vimekidhi vigezo husika.
Mheshimiwa Spika, Serikali itaendelea kupandisha hadhi vituo vya kutolea huduma za afya ambavyo vimekidhi vigezo katika ngazi ya afya ya msingi.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved