Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 42 Information, Communication and Information Technology Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari 543 2025-06-09

Name

Zuberi Mohamedi Kuchauka

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Liwale

Primary Question

MHE FESTO R. SANGA K.n.y. MHE. ZUBERI M. KUCHAUKA aliuliza: -

Je, Serikali ina mpango gani wa kuweka huduma ya bure ya mtandao kwenye vyuo na shule zote nchini?

Name

Maryprisca Winfred Mahundi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, UCSAF imefanikiwa kufikisha internet katika maeneo sita ya umma kikiwemo Chuo cha Maendeleo ya Jamii cha Rungemba (Mafinga), eneo la Bustani ya Nyerere Square (Dodoma), Ndaki ya Habari na Elimu Angavu (Chuo Kikuu cha Dodoma), Soko la Tabora, Kiembe Samaki (Unguja) na Soko la Buhongwa (Mwanza) na maeneo mengine 17 katika viwanja vya maonyesho ya Saba Saba. Lengo la Mradi huu ni kuongeza wigo na matumizi ya mawasiliano ya internet ya kasi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile UCSAF imekuwa ikitekeleza mradi wa kuzipatia shule za Serikali vifaa vya TEHAMA ili kuziunganisha na mtandao wa internet, ambapo mpaka sasa takribani shule 1121 zimenufaika kupitia mradi huu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, utekelezaji wa miradi hii ya kufikisha huduma ya internet katika maeneo ya vyuo na katika shule za Serikali unaendelea kadiri ya upatikanaji wa fedha kwa lengo ya kuzifikia shule zote na maeneo yote yenye uhitaji.