Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 42 Industries and Trade Wizara ya Viwanda na Biashara 541 2025-06-09

Name

Abeid Ighondo Ramadhani

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ilongero

Primary Question

MHE. ABEID R. IGHONDO aliuliza: -

Je, Serikali ina mkakati gani wa kutoa elimu ya Mfumo wa Stakabadhi Ghalani kwa Wakulima ili kuondoa changamoto zilizopo - Singida Kaskazini?

Name

Dr. Selemani Said Jafo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kisarawe

Answer

WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali kupitia Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala (WRRB) na wadau wengine katika Mnyororo wa Mfumo wa Stakabadhi za Ghala ilibaini uwepo wa changamoto ya uelewa kuhusu mfumo unavyofanya kazi kwenye baadhi ya maeneo, hivyo kusababisha kuundwa kwa timu maalum, ili kutoa elimu katika Mikoa ya Singida, Manyara na Dodoma.

Mheshimiwa Mwenyekiti, elimu kuhusu Mfumo wa Stakabadhi za Ghala imetolewa na itaendelea kutolewa katika ngazi ya Halmashauri na Kata zote nchini zinazozalisha mazao mbalimbali, ikiwemo dengu na mbaazi katika Mkoa wa Singida, Jimbo la Singida Kaskazini katika Kata za Mwasauya na Msange.

Mheshimiwa Mwenyekiti, zoezi la utoaji wa elimu kuhusu matumizi ya mfumo huo itakuwa endelevu, ahsante.