Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 42 Home Affairs Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi 540 2025-06-09

Name

Suma Ikenda Fyandomo

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ORAN M. NJEZA K.n.y. MHE. SUMA I. FYANDOMO aliuliza: -

Je, lini Serikali itawapa makoti ya kujikinga na baridi Askari Polisi wanaofanya kazi katika Mkoa wa Mbeya?

Name

Daniel Baran Sillo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Babati Vijijini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, makoti ya kujikinga na baridi ni miongoni mwa sare za Jeshi la Polisi, ambazo Askari wanaofanya kazi kwenye mikoa yenye hali ya hewa ya baridi kali hupatiwa. Mkoa wa Mbeya ni miongoni mwa mikoa ambayo Askari Polisi wanapewa makoti ya kujikinga na baridi kali wakiwa kazini, kama sare ya Jeshi la Polisi. Mikoa mingine inayopewa makoti ya kujikinga na baridi ni Iringa, Njombe, Songwe, Rukwa, Arusha, Manyara, Kilimanjaro pamoja na Wilaya ya Lushoto katika Mkoa wa Tanga, ahsante.