Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 42 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 535 2025-06-09

Name

Selemani Jumanne Zedi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bukene

Primary Question

MHE. SELEMANI J. ZEDI aliuliza: -

Je, lini Serikali itamaliza tatizo la upungufu wa Watumishi wa Kada ya Afya – Bukene?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imeendelea kutoa vibali vya ajira kila mwaka, ambapo kuanzia mwaka wa fedha 2020/2021 hadi 2024/2025 jumla ya watumishi wa kada ya afya 34,720 wameajiriwa na kupangiwa vituo kote nchini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kipindi cha mwaka wa fedha 2020/2021 hadi 2024/2025 Halmashauri ya Wilaya ya Nzega imepangiwa jumla ya watumishi 111, ambao wamepangwa katika Hospitali ya Wilaya, vituo vya afya na zahanati. Kati ya hao, Jimbo la Bukene limepelekewa jumla ya watumishi 59.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali itaendelea kuajiri watumishi wa sekta ya afya kwa awamu na kuwapanga katika maeneo yenye upungufu wa wataalam hao ikiwemo katika Halmashauri ya Wilaya ya Nzega.