Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2020-2025 | Session 19 | Sitting 42 | Regional Administration and Local Government Authorities | Ofisi ya Rais TAMISEMI. | 534 | 2025-06-09 |
Name
Jafari Chege Wambura
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Rorya
Primary Question
MHE. BONIPHACE M. GETERE K.n.y. MHE. JAFARI W. CHEGE aliuliza: -
Je, lini ujenzi wa Kituo cha Afya Rabour - Rorya utakamilika?
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka wa fedha 2021/2022 Kituo cha Afya cha Rabour kilipokea jumla ya shilingi milioni 530 kwa ajili ya ujenzi wa jengo la kuhudumia wagonjwa wa nje (OPD), jengo la maabara, jengo la wazazi na jengo la kupasulia wagonjwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, hadi kufikia Mei, 2025, majengo matatu yamekamilika na huduma za wagonjwa wa nje na maabara zinatolewa. Aidha, jengo la upasuaji na jengo la kufulia ujenzi wake umefikia 80%.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali itaendelea kutenge fedha kwa awamu kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa vituo vya afya kote nchini kikiwemo Kituo cha Afya cha Rabour.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved