Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2020-2025 | Session 19 | Sitting 17 | Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives | Wizara ya Kilimo | 222 | 2025-05-05 |
Name
Maimuna Salum Mtanda
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Newala Vijijini
Primary Question
MHE. MAIMUNA S. MTANDA aliuliza:-
Je, Serikali ina mpango gani wa kutumia redio za kijamii kutoa elimu ya matumizi bora ya viuatilifu katika zao la korosho?
Name
David Ernest Silinde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduma
Answer
NAIBU WAZIRI WA KILIMO alijibu:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mikoa inayozalisha korosho, vituo kumi na moja vya redio jamii vinatoa huduma kwa wakulima, hususani teknolojia mbalimbali. Mathalani, mwezi Februari hadi Machi, 2024 tangazo la kuhuisha taarifa kwenye kanzidata inayotumika kusajili na kugawa pembejeo za ruzuku za zao la korosho lilitolewa kupitia Redio za Fadhila FM, Mercy FM, Mamu FM na Safari FM. Vilevile, mwezi Agosti hadi Septemba, 2024 kupitia redio Newala FM na Rufiji FM zilitumika kutoa tahadhari na udhibiti wa ugonjwa wa blight kwa wakulima wa Korosho katika Mikoa ya Lindi na Pwani.
Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na matumizi ya redio za jamii, Wizara ya Kilimo imeanzisha Kituo cha Huduma kwa Wateja kinachotoa fursa kwa wakulima na wadau wengine wa kilimo kupata elimu na ufafanuzi kuhusu maendeleo ya kilimo ikiwemo zao la korosho.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved