Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 17 Information, Culture, Arts and Sports Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo 221 2025-05-05

Name

Nusrat Shaaban Hanje

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. NUSRAT S. HANJE aliuliza:-

Je, Serikali inafanya maandalizi gani kuhakikisha nchi yetu inafanya vizuri katika Mashindano ya AFCON 2027?

Name

Hamis Mohamed Mwinjuma

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Muheza

Answer

NAIBU WAZIRI WA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inaendelea na ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya michezo katika Majiji ya Dar es Salaam, Arusha, Dodoma na Visiwani Zanzibar, kwa ajili ya kufanikisha mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON, 2027) yanayotarajiwa kufanyika nchini kwa kushirikiana na Nchi za Kenya na Uganda. Aidha, kupitia Baraza la Michezo la Taifa (BMT) na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) tunasimamia malezi ya timu ya vijana kimkakati ili kuhakikisha tunakuwa na timu bora yenye viwango wa ushindani wa kimataifa. Baadhi ya masuala yaliyofanyika ni pamoja na kuanzisha programu za kuendeleza vipaji kwa kuzishirikisha timu za vijana waliochini ya miaka 17, waliochini ya miaka 23 na kutumia wachezaji wa diaspora.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mipango mingine ni kuboresha mikakati ya upatikanaji wa vifaa mbalimbali vya michezo, kuandaa benchi la ufundi lililo bora, kuandaa programu za lishe, kuandaa kambi za mazoezi ya muda mrefu, kuandaa michezo ya kirafiki ya kimataifa na kuboresha na kusimamia maslahi ya wachezaji.