Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 35 Energy and Minerals Wizara ya Nishati 449 2025-05-29

Name

Eng. Stella Martin Manyanya

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Nyasa

Primary Question

MHE. ENG. STELLA M. MANYANYA aliuliza:-

Je, hatua gani imefikiwa kupeleka umeme Kitongoji cha Songea Pori na Nindi vinavyopakana na Msumbiji kama ilivyoahidiwa na Serikali?

Name

Judith Salvio Kapinga

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA NISHATI alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Kitongoji cha Songea Pori kilichopo katika Kijiji cha Lunyele, Kata ya Mpepo na Kitongoji cha Nindi kilichopo Kijiji cha Konganywita, Kata ya Mipotopoto vilifanyiwa upembuzi yakinifu na kubaini kwamba, vinahitaji kuwekewa njia za kusambaza umeme za msongo wa kati kwa umbali wa kilometa tatu.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inatarajia kuvipelekea umeme vitongoji hivi kupitia Mradi wa Kupeleka Umeme Vitongojini Awamu ya Pili “B” ambao utekelezaji wake utaanza mwaka huu wa fedha 2025/2026. Kwa sasa taratibu za kuwapata wakandarasi zinaendelea, ahsante.