Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 35 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 448 2025-05-29

Name

Ally Juma Makoa

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kondoa Mjini

Primary Question

MHE. ALLY J. MAKOA aliuliza: -

Je, Serikali ina mpango gani wa kuongeza Walimu wa Shule za Msingi na Sekondari katika Jimbo la Kondoa Mjini?

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA) alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, Halmashauri ya Kondoa Mji ina mahitaji ya walimu 674 (msingi 414 na sekondari 260), waliopo ni 450 (msingi 266 na sekondari 184) na upungufu ni walimu 224 (msingi 148 na sekondari 76).

Mheshimiwa Naibu Spika, mwaka 2024/2025 Serikali imeajiri walimu 15,925 wa shule za msingi na shule za sekondari ambapo Halmashauri ya Kondoa Mji ilipangiwa walimu 33 (msingi saba na sekondari 26).

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali itaendelea kuajiri walimu na kuwapangia vituo vya kazi katika maeneo yenye uhitaji mkubwa. (Makofi)