Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 35 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 447 2025-05-29

Name

Mwanaisha Ng'anzi Ulenge

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. RASHID A. SHANGAZI K.n.y. MHE. ENG. MWANAISHA N. ULENGE aliuliza: -

Je, upi mkakati wa kuzitengeneza barabara za Mkoa wa Tanga zilizopo TARURA zilizofunguliwa kwa fedha za tozo na fedha zilizopelekwa Jimboni?

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA) alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imeongeza bajeti Mkoa wa Tanga kutoka shilingi bilioni 12.4 hadi shilingi bilioni 37.1 ambapo kupitia fedha hizi, baadhi ya barabara zimeweza kufunguliwa, kujengwa kutoka changarawe hadi lami, na barabara za udongo kuwa changarawe. Aidha, barabara zilizosajiliwa ndizo zenye uhalali wa kufanyiwa matengenezo kwa kutumia fedha zinazotolewa na Mfuko wa Barabara.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imeongeza barabara za lami kutoka kilomita 124.078 hadi kilomita 165.68 na kuongeza barabara za changarawe kilomita 2,104.25, ambapo kati ya hizo zipo ambazo zilikuwa zimesajiliwa na zinaendelea kufanyiwa matengenezo kwa kutumia fedha kutoka Mfuko wa Barabara.

Mheshimiwa Naibu Spika, hadi sasa, takribani kilomita 1,486.4 za barabara ambazo hazijasajiliwa, tayari Serikali imeshaanza mchakato wa kuzisajili ili zitambulike na kuweza kutengewa fedha kwa ajili ya matengenezo ya mara kwa mara (Routine Maintenance) kwa kutumia fedha za Mfuko wa Barabara.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali itaendelea kuihudumia miundombinu ya barabara na madaraja ya Mkoa wa Tanga kwa kujenga, kukarabati na kutengeneza kulingana na upatikanaji wa fedha. (Makofi)