Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Ibrahim Mohamed Shayo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Moshi Mjini
Primary Question
MHE. IBRAHIM M. SHAYO aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kuboresha au kujenga nyumba za kisasa za TBA Manispaa ya Moshi?
Supplementary Question 1
MHE. IBRAHIM M. SHAYO: Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na majibu mazuri ya Serikali, naomba kuuliza maswali madogo mawili ya nyongeza. Kwa kuwa, wananchi wamekaa kwenye yale makazi takribani miaka 40, je, Serikali haioni sasa kuna haja ya kuwamilikisha au baada ya ujenzi kuwapa nyumba moja moja?
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili. Katika ujenzi huo, Serikali haioni kuna sababu ya kushirikisha wadau (PPP) kwenye ujenzi wa nyumba hizo?
Name
David Mwakiposa Kihenzile
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mufindi Kusini
Answer
NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI K.n.y. WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninampongeza Mheshimiwa Shayo kwa kuwapenda wananchi wake na kuwasemea wapangaji mbalimbali nchi nzima ambao wapo kwenye nyumba za TBA.
Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na maswali yake ya msingi, naomba ni mpe majibu kwamba, anasema wapangaji wamekaa miaka 30 kwenye nyumba hizo, kwa hiyo, pengine wapewe kipaumbele.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli wamekaa miaka hiyo 30 au 40 na zaidi, lakini wanalipa kodi, kwa hiyo wanakuwa na haki sawa na Watanzania wengine. Haina maana kwamba kwa kukaa kwao sasa ndiyo wamilikishwe au wapewe rasilimali hizo za Taifa zima.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakubaliana na Mheshimiwa Mbunge, lakini kama ambavyo nimesema, TBA ipo kwenye mpango wa kufanya maendelezo ya shirika letu na kuboresha nyumba zetu. Pindi ujenzi utakapokuwa unafanywa, Serikali inatambua umuhimu wa kutoa kipaumbele kwa wapangaji ambao wapo ndani kwa sasa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake la pili, amezungumza kuhusu kuzishirikisha sekta binafsi. Wakala wa Majengo (TBA) imeshaanza mchakato huo wa kuhuisha sheria na taratibu za kuanzishwa kwake, ambapo kupitia Gazeti Na. 595 tumeona maboresho ambayo yamefanywa kwenye sheria zetu, na ambapo tayari imetoa fursa ya kuanza kushirikisha sekta binafsi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, hili Mheshimiwa Waziri wa Ujenzi ameniambia niwahakikishie kwamba, kama ilivyo taasisi nyingine, na kama ulivyo uelekeo wa nchi kuelekea kwenye dira yetu ya 2050, ushiriki wa sekta binafsi katika kushika na kujenga uchumi wetu haujadiliki tena. Hivyo basi, tayari maeneo 149 yamekwishatambuliwa, ambapo sekta binafsi itakwenda kushirikishwa katika uendelezaji wa nyumba hizo za Serikali.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved