Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Joshua Samwel Nassari
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Arumeru-Mashariki
Primary Question
MHE. JOSHUA S. NASSARI aliuliza: - Je, lini Serikali itatoa fedha, ili kukamilisha miradi mikubwa ya maji, Meru, iliyosimama, ili kuondoa shida kubwa ya maji kwa wananchi?
Supplementary Question 1
MHE. JOSHUA S. NASSARI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninashukuru nimepata access ya mic. Pia ninashukuru kwa majibu mazuri ya Serikali, lakini niseme tu kwamba, sisi watu wa Wilaya ya Arumeru, ambao tupo chini ya Mlima Meru, nadhani siyo sawa sana kwamba, maji yanatoka kwetu yanakwenda Monduli, yanatoka kwetu yanakwenda Arusha Mjini na maeneo mengine, halafu sisi ambao tunatunza vyanzo vya maji bado kuna watu wetu hawana maji.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa Mheshimiwa Waziri amesema hapo kwamba, miradi imesimama labda kwa kukosa fedha na nini, lakini kwa sababu ya flow ya fedha, kwa miradi ambayo Serikali imetoa fedha ila mkandarasi anasuasua, kwa mfano mkandarasi mkubwa wa Kikatiti – Samaria, mkandarasi anaitwa Help Desk, amepewa fedha, lakini bado anasuasua.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tumechunguza tukakuta huyo mkandarasi ana miradi mingi, kwa hiyo, ni kama vile anaelemewa. Halikadhalika, mradi mdogo wa hapo Imbaseni ambao unakwenda kutoa relief ambao upo chini ya Mamlaka ya AUWSA na wenyewe umefika mbali na Serikali imetoa fedha, lakini sijui kwa nini unasuasua kukamilika.
MWENYEKITI: Swali.
MHE. JOSHUA S. NASSARI: Mheshimiwa Mwenyekiti, maswali yangu kwa Serikali. La kwanza, Serikali ipo tayari leo hii kufuatilia kwa hao watu wa AUWSA na yule bwana Help Desk, ili miradi ile iweze kukwamuka na kwenda mbele?
Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili ni ombi. Waziri wa Maji, ndugu yangu Mheshimiwa Juma Aweso hapo, ananisikiliza na ninajivuna kwamba mimi nilimpokea Form One Mwaka 2001 pale Bagamoyo Sekondari, na leo ni Mheshimiwa Waziri wetu wa Maji. Sasa, yupo tayari kuambatana na mimi ndugu yangu, twende kule Meru, ili tukaangalie miradi ya Uwiro, Shambarai na kwingineko, ambayo ni kama imesuasua, ili tuweze kuikwamua? Nashukuru sana.
Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi Mjini
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninampongeza sana Mheshimiwa Mbunge kwa ufuatiliaji wa karibu. Ninakiri kwamba, tangu jana amekuwa akifuatilia, na leo hii amenijulia kabisa kwamba, atamwomba Waziri wa Maji, Mheshimiwa Jumaa Hamidu Aweso, aongozanenaye na baada ya kuniambia nijibu moja kwa moja kwenye suala hilo, niliongea na Mheshimiwa Waziri akasema kwamba, yeye mwenyewe atanyanyuka kwenda mpaka katika Jimbo la Mheshimiwa Nassari kuhakikisha kwamba changamoto ambazo zinajitokeza katika eneo hilo, basi zinachukuliwa hatua.
Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile picha nzima ya Arumeru Mashariki ni kwamba tunavyo vijiji 90, lakini katika vijiji 90 hivyo vijiji 52 vina huduma safi kabisa ya majisafi na salama. Tunatambua kwamba, kuna vijiji 30 ambavyo hali yake siyo ya kuridhisha sana. Tunafahamu pia, vijiji vinane hivyo ndivyo ambavyo havina mifumo rasmi ya utoaji wa huduma ya majisafi na salama.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninamtoa hofu Mheshimiwa Mbunge, katika vijiji 1,575 vilivyobaki nchi nzima vijiji vyake vinane tutaviingiza katika programu hiyo, ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya majisafi na salama.
Mheshimiwa Mwenyekiti, pia, tunao mradi ambao umekamilika. Mradi wa Patandi ambao ni wa shilingi bilioni 3.125 tayari umeanza kutoa huduma ya majisafi na salama. Pia, Mradi wa Imbeseni tayari umeanza kutekelezwa. Tenki la lita 1,000,000 limekamilika, intake structure tumekamilisha na pia tunalaza mabomba. Kutoka kwenye chanzo kwenda kwenye bomba pale tumebakiza meta 500.
Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile tunafamu kabisa kwamba, distribution line ambayo inatakiwa ni kilometa 14, kilometa nne tumekamilisha, sasa tupo kwenye hatua za mwishoni kuhakikisha kwamba, mradi huu unakamilika na wananchi wa maeneo ya Imbaseni wanapata huduma ya majisafi na salama.
Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na miradi mingine yote ambayo ipo, minane katika Jimbo la Mheshimiwa Nassari, ina gharama ya shilingi bilioni 10.147, ambapo ni uwekezaji mkubwa sana wa Serikali ya Awamu ya Sita, chini ya Uongozi wa Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan. Nakushukuru sana.
Name
Jonas William Mbunda
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mbinga Mjini
Primary Question
MHE. JOSHUA S. NASSARI aliuliza: - Je, lini Serikali itatoa fedha, ili kukamilisha miradi mikubwa ya maji, Meru, iliyosimama, ili kuondoa shida kubwa ya maji kwa wananchi?
Supplementary Question 2
MHE. JONAS W. MBUNDA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Serikali ilianza kujenga Mradi wa Maji katika Kijiji cha Pachasita, Kata ya Kiungu, Jimbo la Mbinga Mjini, lakini sasa ni muda mrefu mradi huo haujakamilika. Nini mpango wa Serikali kuhakikisha kwamba, inakamilisha mradi huu na wananchi waweze kupata maji?
Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi Mjini
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kabisa Serikali inayo miradi inayoendelea kutekelezwa nchi nzima. Zaidi ya miradi 867 ambayo ipo katika hatua mbalimbali za utekelezaji na gharama nzima ya kuhakikisha kwamba miradi hii inakamilika, ni zaidi ya shilingi trilioni 1.3.
Mheshimiwa Mwenyekiti, lazima tuhakikishe kwamba, miradi hii tunaitenga kwa makundi mbalimbali, kama ambavyo nimejibu katika majibu ya jana hapa kuwa, miradi ambayo imekaribia ukingoni kukamilika kabisa, hiyo ndiyo tunaipa kipaumbele ikamilike, baadaye tunashuka katika hatua za katikati, then tunashuka katika miradi ya chini.
MWENYEKITI: Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, tutahakikisha kwamba, pia mradi wa Mheshimiwa Mbunge, na wenyewe unaingizwa katika vipaumbele hivyo, ili tuweze kuhakikisha kwamba, unakamilika na kutoa huduma ya majisafi na salama.
Name
Japhet Ngailonga Hasunga (CPA)
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Vwawa
Primary Question
MHE. JOSHUA S. NASSARI aliuliza: - Je, lini Serikali itatoa fedha, ili kukamilisha miradi mikubwa ya maji, Meru, iliyosimama, ili kuondoa shida kubwa ya maji kwa wananchi?
Supplementary Question 3
MHE. JAPHET N. HASUNGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Mradi wa maji wa kutoka Mafumbo ambao tunatarajia uweze kuhudumia Mji wa Vwawa, wenye thamani ya shilingi bilioni saba, una zaidi ya miaka mitatu toka mkataba usainiwe, na fedha hazijaenda. Ni lini Serikali itapeleka fedha hizo?
Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi Mjini
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kama ambavyo nimesema katika jibu lililopita, miradi tunayo mingi inayoendelea kutekelezwa. Tutahakikisha mradi wake tunaupatia kipaumbele kuhakikisha kwamba, mkandarasi analipwa ili uweze kukamilika kwa wakati. Ahsante sana.
Name
Festo Richard Sanga
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Makete
Primary Question
MHE. JOSHUA S. NASSARI aliuliza: - Je, lini Serikali itatoa fedha, ili kukamilisha miradi mikubwa ya maji, Meru, iliyosimama, ili kuondoa shida kubwa ya maji kwa wananchi?
Supplementary Question 4
MHE. FESTO R. SANGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninajua unafahamu kwamba swali hili ni moja kati ya maswali yaliyoulizwa mara nyingi zaidi Bungeni, watu wa kitengo cha ufuatiliaji wanakwambia. Ni lini mtakamilisha Mradi wa Mpungi wa zaidi ya shilingi milioni 800? Fedha ndogo tu, lakini zaidi ya miaka minne mradi haujakamilika na mkandarasi tulisaini mkataba.
Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi Mjini
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Mbunge ameendelea kuuliza kuhusu hili swali, na ninafahamu kuna miradi mingi katika eneo lake. Kuna mradi ule wa Ikonda, Usalimwani, kuna ule Mradi wa Kitope, Kigulu, pamoja na hiyo ambayo ameitaja.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninafahamu kwamba, mahitaji yake ni fedha. Nimtoe hofu Mheshimiwa Mbunge, sisi kama Wizara, tunaendelea kuchakata na kuweka tathmini miradi ipi tuipe kipaumbele ili tuhakikishe inakamilika kwanza, halafu baadaye mingine inaendelea.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakutoa hofu na miradi yako tutaingiza katika vipaumbele. Ahsante sana.
Name
Emanuel Qambaji Nuwas
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mbulu Vijijini
Primary Question
MHE. JOSHUA S. NASSARI aliuliza: - Je, lini Serikali itatoa fedha, ili kukamilisha miradi mikubwa ya maji, Meru, iliyosimama, ili kuondoa shida kubwa ya maji kwa wananchi?
Supplementary Question 5
MHE. DKT. EMANUEL Q. NUWAS: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi hii ya kuuliza swali dogo la nyongeza. Mheshimiwa Naibu Waziri kuna Mradi wa Kutibu Maji Taka katika Halmashauri ya Mji wa Babati ambao ni mabwawa manne. Je, lini Serikali itapeleka fedha za kukamilisha mradi huo, ili kuwasaidia wananchi wa Halmashauri ya Mji wa Babati?
Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi Mjini
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, Mradi wa Majitaka wa Babati tumeuweka kwenye vipaumbele vya kupelekea fedha katika kipindi hiki cha bajeti.
Name
Faraji Buriani Nandala
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ndanda
Primary Question
MHE. JOSHUA S. NASSARI aliuliza: - Je, lini Serikali itatoa fedha, ili kukamilisha miradi mikubwa ya maji, Meru, iliyosimama, ili kuondoa shida kubwa ya maji kwa wananchi?
Supplementary Question 6
MHE. FARAJI B. NANDALA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipatia nafasi, ili nami niweze kuuliza swali la nyongeza. Ni lini Serikali itapeleka fedha kwa ajili ya kuanza ujenzi wa chujio kwenye chanzo cha Mbwinji kwa kuzingatia kwamba, chanzo hiki ni muhimu sana kwa majimbo manne, yaani Ndanda, Masasi, Nanyumbu na Nachingwea?
Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi Mjini
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imejipanga kuhakikisha kwamba, maeneo ambayo ni ya kujenga chujio, maana yake ni maeneo ambayo ni ya kutibu maji, kuyafanya yawe safi na salama. Haya ni maeneo yenye kipaumbele ambayo Mheshimiwa Waziri ameweka msisitizo, na tutahakikisha kwamba, eneo alilolitaja Mheshimiwa Mbunge pia tutalipelekea fedha, ili mradi huu uweze kujengwa kwa haraka sana. Ahsante sana.
Name
Zacharia Paulo Issaay
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mbulu Mjini
Primary Question
MHE. JOSHUA S. NASSARI aliuliza: - Je, lini Serikali itatoa fedha, ili kukamilisha miradi mikubwa ya maji, Meru, iliyosimama, ili kuondoa shida kubwa ya maji kwa wananchi?
Supplementary Question 7
MHE. ZACHARIA P. ISSAAY: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana. Hivi sasa kuna Miradi ya Visima Sita katika Jimbo la Mbulu Mjini ambavyo vimesimama kwa muda mrefu. Je, ni lini Serikali itawalipa wakandarasi wale ili waweze kurudi site na kukamilisha miradi hiyo ya visima?
Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi Mjini
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kabisa tunakiri kwamba, mkandarasi amekuwa na changamoto katika mradi huo. Bahati nzuri, kwenye ziara ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, tulishirikiana na Mheshimiwa Mbunge katika kujadiliana namna bora ya kufanya ili mkandarasi arudi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninamtoa hofu, tupo katika hatua nzuri za kuhakikisha kwamba mkandarasi anarudi na kutekeleza mradi vizuri sana.
Name
Dotto Jasson Bahemu
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ngara
Primary Question
MHE. JOSHUA S. NASSARI aliuliza: - Je, lini Serikali itatoa fedha, ili kukamilisha miradi mikubwa ya maji, Meru, iliyosimama, ili kuondoa shida kubwa ya maji kwa wananchi?
Supplementary Question 8
MHE. DOTTO J. BAHEMU: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. katika Jimbo letu la Ngara, kuna Kata mbili, Murusagamba na Nyamagoma, ambapo kuna Vijiji vya Ntanga na Kumubuga, ambapo tuna Mradi wa Maji wa muda mrefu ambao ulikuwa unatekelezwa pale, lakini baadaye mkandarasi ni kama ameutelekeza kwa muda mrefu, sasa imefikia hatua wananchi wa vile vijiji...
MWENYEKITI: Uliza swali.
MHE. DOTTO J. BAHEMU: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni sababu zipi ambazo zimesababisha ule mradi kusimama, na lini Serikali itaendeleza ule mradi, ili wananchi wa Ntanga na Kumubuga wapate majisafi na salama? Ahsante.
MWENYEKITI: Majibu.
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, Samahani. Sijamsikia vizuri.
MWENYEKITI: Uliza hapo mwishoni kwa kifupi.
MHE. DOTTO J. BAHEMU: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni lini Serikali itafuatilia kujua sababu za Mradi wa Maji wa Kumubuga na Ntanga kusimama ili uweze kufanya kazi na wananchi wa vijiji vile wapate maji safi na salama?
Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi Mjini
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la Mheshimiwa Mbunge ni lini tutafuatilia?
Mheshimiwa Mwenyekiti, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba kuanzia leo tunafuatilia kujua sababu ambazo zimesababisha mkandarasi kutoendelea na mradi. Ahsante sana.
Name
Alan Thomas Mvano
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kakonko
Primary Question
MHE. JOSHUA S. NASSARI aliuliza: - Je, lini Serikali itatoa fedha, ili kukamilisha miradi mikubwa ya maji, Meru, iliyosimama, ili kuondoa shida kubwa ya maji kwa wananchi?
Supplementary Question 9
MHE. ALAN T. MVANO: Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na jitihada nzuri za Serikali, bado kuna wananchi wanapata shida ya maji katika Wilaya ya Kanonko. Ni lini Serikali itaanza ujenzi wa mradi wa maji katika Vijiji vya Juhudi na Kazilamihunda ndani ya Kata ya Kasanda? (Makofi)
Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi Mjini
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, Kata ya Kasanda Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira pale Kakonko tayari wameshatangaza tender ya kumpata mkandarasi ambaye ataenda kutekeleza mradi huu wa Kata ya Kasanda. Nimtoe hofu, tuendelee kusubiri mchakato mzima wa kumpata mkandarasi. Utakapokamilika tu, mkandarasi ataingia site na kuanza kutekeleza mradi huo, ahsante sana.
Name
Mwita Mwikwabe Waitara
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tarime Vijijini
Primary Question
MHE. JOSHUA S. NASSARI aliuliza: - Je, lini Serikali itatoa fedha, ili kukamilisha miradi mikubwa ya maji, Meru, iliyosimama, ili kuondoa shida kubwa ya maji kwa wananchi?
Supplementary Question 10
MHE. MWITA M. WAITARA: Mheshimiwa Mwenyekiti, mradi wa maji Kata ya Nyanungu unahudumia Kata ya Gorong’a na Nyanungu yenyewe ina jumla ya vijiji nane na vitongoji zaidi ya 30. Mradi huu umesimama, mkandarasi hajalipwa na pump haijanunuliwa. Je, nini kauli ya Serikali juu ya eneo hilo ili wananchi waweze kupata majisafi na salama? Ahsante.
Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi Mjini
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninampongeza sana Mheshimiwa Mwita Waitara kwa kufuatilia kwa ukaribu sana miradi ya vijiji vinane, na bahati nzuri jana, mimi, pamoja na Mheshimiwa Mbunge pamoja na wataalam wa RUWASA tulikaa kikao na tukakubaliana. Yale ambayo tumekubaliana ni kuhakikisha tunapeleka fedha na kuhakikisha mkandarasi anaendelea kutekeleza miradi hiyo na katika vijiji ambavyo Mbunge aliviomba na vyenyewe tunaviingiza kwenye mpango kuhakikisha kwamba wanapata huduma ya majisafi na salama.
Name
Edwin Enosy Swalle
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Lupembe
Primary Question
MHE. JOSHUA S. NASSARI aliuliza: - Je, lini Serikali itatoa fedha, ili kukamilisha miradi mikubwa ya maji, Meru, iliyosimama, ili kuondoa shida kubwa ya maji kwa wananchi?
Supplementary Question 11
MHE. EDWIN E. SWALLE: Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Naibu Waziri alikuja Jimbo la Lupembe, Kata ya Kichiwa ambayo ina Mradi wa Maduma, Kichiwa mpaka Takamenda. Mradi huu umejengwa kwa zaidi ya 80% na hivi sasa umekwama kwa sababu hatuna fedha takribani milioni 400. Mheshimiwa Naibu Waziri, ni lini fedha hii shilingi milioni 400 itakuja huu mradi uanze kufanya kazi? Ahsante.
Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi Mjini
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninapenda kujibu swali la Mheshimiwa Wakili Msomi, Mheshimiwa Swalle, Mbunge, kuhusu mradi huu wa Chiwa. Ni kweli kabisa nilifika katika mradi huu, na mradi huu utekelezaji wake uko kati ya 80% na 85%. Kama ambavyo nimejibu hapa, miradi ambayo imefika ukingoni msisitizo wa Mheshimiwa Waziri wa Maji ni kupeleka fedha kwa haraka sana.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninamtoa hofu kwa sababu Mheshimiwa Waziri yuko hapa pia anasikia, tutahakikisha tunapeleka fedha na mradi huo ukamilike kama ambavyo umekusudiwa. Ahsante sana.
Name
Emanuel Qambaji Nuwas
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mbulu Vijijini
Primary Question
MHE. JOSHUA S. NASSARI aliuliza: - Je, lini Serikali itatoa fedha, ili kukamilisha miradi mikubwa ya maji, Meru, iliyosimama, ili kuondoa shida kubwa ya maji kwa wananchi?
Supplementary Question 12
MHE. DKT. EMANUEL Q. NUWAS: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa kupata nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Katika Jimbo la Mbulu Vijijini tuna mradi wa Dambia ambao unahudumia vijiji 21, Mkandarasi amesha-raise certificate ya malipo na sasa anadai karibu shilingi bilioni 1.7. Je, Serikali ina mpango gani wa kumlipa mkandarasi ili aendelee na kazi? (Makofi)
Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi Mjini
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kabisa mradi huu mkandarasia amewasilisha hati za madai. Mradi huu pia ulitembelewa na Kamati yetu ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira. Ni mradi ambao tumeupa kipaumbele ambao unaenda kuhudumia wakazi wengi sana.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, tunaendelea na mchakato wa kuhakikisha kwamba Mkandarasia analipwa ili arudi kutekeza mradi kwa haraka zaidi kama ambavyo imekusudiwa, ahsante sana.
Name
Azza Hilal Hamad
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. JOSHUA S. NASSARI aliuliza: - Je, lini Serikali itatoa fedha, ili kukamilisha miradi mikubwa ya maji, Meru, iliyosimama, ili kuondoa shida kubwa ya maji kwa wananchi?
Supplementary Question 13
MHE. AZZA H. HAMAD: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa na nafasi niweze kuuliza swali la nyongeza. Kwa kuwa mradi wa maji ya Ziwa Victoria unaotakelezwa katika Kijiji cha Ibanza na Kijiji cha Mwamala ndani ya Jimbo la Itwangi, umesimama takribani mwaka mmoja na nusu sasa mkandarasi akidai fedha zake milioni 100 tu, je, Waziri haoni kuna sababu ya msingi kumlipa mkandarasi huyu hili wananchi waondokane na adha kubwa ya maji wanayoipata? (Makofi)
Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi Mjini
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninampongeza sana Dada yangu Mheshimiwa Azza kwa kuendelea kuwasemea wananchi wa Itwangi na kuendelea kuisimamia falsafa ya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kumtua Mama ndoo kichwani. Sababu za msingi kabisa za kumlipa mkandarasi ni kuhakikisha wananchi wa Itwangi wanapata huduma ya majisafi na salama.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tutaharakisha malipo ya mkandarasi ili aweze kulipwa na kuhakikisha kwamba mradi unakamilika, ahsante sana.