Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Josephine Joseph Kapoma

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. JOSEPHINE J. KAPOMA aliuliza: - Je, Serikali ina mkakati gani wa kufikisha elimu kwa wananchi kuhusu Biashara ya Hewa ya Ukaa kwa kuwa ni miongoni mwa biashara kubwa duniani?

Supplementary Question 1

MHE. JOSEPHINE J. KAPOMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninashukuru kwa majibu mazuri ya Serikali. Sasa naomba niulize maswali mawili ya nyongeza. Je, Serikali inasimamia vipi kuhakikisha vijiji husika vinapata magawio yao kwa usawa?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili. Takwimu inaonesha kampuni nyingi za wanunuzi wa hewa ya ukaa ni kampuni za kigeni. Je, Serikali imeweka vigezo rafiki kuvutia kampuni za wawekezaji wazawa? (Makofi)

Name

Kwagilwa Reuben Nhamanilo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Handeni Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MUUNGANO NA MAZINGIRA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nimpongeze sana Mheshimiwa Mbunge Josephine, amekuwa ni msemaji mzuri wa kuutetea mkoa mzima wa Morogoro na Watanzania kwa ujumla.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ameuliza maswali mawili ya nyongeza. La kwanza, ni kwa namna gani Serikali inahakikisha vijiji vinapata magawio sawia kwenye biashara hii ya hewa ya ukaa? Serikali imeweka utaratibu wa kikanuni na wa kimiongozo kupitia Kituo chetu cha Uratibu wa Biashara hii ya Kaboni (NCMC) kwamba, biashara inapokuwa imefanyika, kijiji hupata 50% kama biashara hii imefanyika kwa kupitia uvunaji wa hewa ya ukaa kwa kupitia misitu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vivyo hivyo, halmashauri husika, kama kampuni iliyofanya biashara ni kampuni ya kigeni, italazimika kulipa 10% kwenye halmashauri hiyo, na vilevile kampuni hiyo italazimika kulipa asilimia moja kwenye mkoa husika.
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake la pili ni lilikuwa kwamba kampuni nyingi zinazofanya shughuli ya ununuzi wa credit zinazotokana na biashara hii ya hewa ya ukaa ni za kigeni. Ametaka kujua ni mkakati gani uliopo wa kuwafanya wazawa waweze kuwa wanunuzi kama ambavyo kampuni za kigeni zinanunua?

Mheshimiwa Mwenyekiti, hii ni biashara ambayo kwa ngazi ya ununuzi inahitaji mtaji mkubwa. Sisi kama Serikali tunaandaa mwongozo na mkakati maalumu wa namna ya kuwawezesha Watanzania wazawa ili waweze kuwa na mitaji ya kuweza kununua credits hizi za kaboni, waweze kushiriki kwenye biashara hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vivyo hivyo, kwenye miongozo hii na mikakati tunayoiandaa kupitia Kituo chetu cha NCMC tunaweka utaratibu wa kushirikisha sekta binafsi na hususan benki, ili ziweze kushiriki kuwawezesha Watanzania wazawa kimitaji. Kama ambavyo tumeona benki zikifanya kwenye maeneo mengine kama ilivyokuwa kwenye barabara, benki zimefanya kwenye infrastructure bond. Kwa hiyo, vivyo hivyo, hata kwenye eneo hilo la hewa ya ukaa Serikali itakwenda na uelekeo huo.

Name

Abdul Yussuf Maalim

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Amani

Primary Question

MHE. JOSEPHINE J. KAPOMA aliuliza: - Je, Serikali ina mkakati gani wa kufikisha elimu kwa wananchi kuhusu Biashara ya Hewa ya Ukaa kwa kuwa ni miongoni mwa biashara kubwa duniani?

Supplementary Question 2

MHE. ABDUL YUSSUF MAALIM: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Zanzibar inanufaika vipi na biashara ya hewa ya ukaa ikiwa ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania? (Makofi)

Name

Kwagilwa Reuben Nhamanilo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Handeni Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MUUNGANO NA MAZINGIRA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninapenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Abdul Yussuph, Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutoka Zanzibar.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imeweka utaratibu mzuri wa kuimarisha masuala yote ya Muungano pamoja na masuala yote ya ushirikiano baina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar. Tumekuwa tukishirikiana kwenye masuala mengi ikiwepo kwenye miradi ya TASAF, miradi ya elimu kupitia mamlaka ya elimu. Vivyo hivyo, na kwenye miradi yote inayohusisha uhifadhi wa mazingira, Zanzibar imekuwa ikishirikishwa na miradi hii tunaitekeleza kote Tanzania Bara na Visiwani. (Makofi)

Name

Thomas Maganga Kampala

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Katavi

Primary Question

MHE. JOSEPHINE J. KAPOMA aliuliza: - Je, Serikali ina mkakati gani wa kufikisha elimu kwa wananchi kuhusu Biashara ya Hewa ya Ukaa kwa kuwa ni miongoni mwa biashara kubwa duniani?

Supplementary Question 3

MHE. THOMAS K. MAGANGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na kuziwezesha kampuni za Kitanzania mitaji, biashara hii ya kaboni inahitaji teknolojia kubwa sana. Je, ni upi mkakati wa Serikali kuwawezesha wananchi na kampuni za kizawa kuingia kwenye biashara hii kulingana na teknolojia ilivyo kubwa?

Name

Kwagilwa Reuben Nhamanilo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Handeni Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MUUNGANO NA MAZINGIRA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nilivyojibu kwenye swali la msingi la kwenye swali la nyongeza ambalo limetangulia kuulizwa. Serikali kupitia Kituo chetu cha NCMC (National Carbon Monitoring Centre) tunaandaa mkakati maalumu wa kuwawezesha Watanzania kwenye eneo hili la ununuzi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye eneo la uwekezaji, tayari Watanzania wanashiriki, hata vijiji vinashiriki kupitia misitu ambayo wamehifadhi, lakini vivyo hivyo, hata kama Mtanzania ana msitu wake binafsi, taratibu zinamruhusu kuanza uwekezaji wa kuvuna credits za kaboni ili waweze kushiriki biashara hiyo.

Name

Zuberi Yahya Mfaume

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Morogoro Kusini

Primary Question

MHE. JOSEPHINE J. KAPOMA aliuliza: - Je, Serikali ina mkakati gani wa kufikisha elimu kwa wananchi kuhusu Biashara ya Hewa ya Ukaa kwa kuwa ni miongoni mwa biashara kubwa duniani?

Supplementary Question 4

MHE. ZUBERI Y. MFAUME: Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Naibu Waziri, Jimbo la Morogoro Kusini sehemu kubwa ni misitu. Ni lini sasa vijiji vyetu vitasajiliwa kuanza kuuza rasmi hewa ya ukaa?

Name

Kwagilwa Reuben Nhamanilo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Handeni Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MUUNGANO NA MAZINGIRA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninapenda kujibu swali la Mheshimiwa Zuberi Mfaume, Mbunge wa Morogoro Kusini na Makamu Mwenyekiti wetu wa Kamati ya Sheria Ndogo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kwamba Mkoa wa Morogoro na hususan Jimbo la Morogoro Kusini lina misitu mingi. Utaratibu uliopo ni kwamba kama misitu hii ipo chini ya vijiji, na kwa maana hiyo iko chini ya halmashauri, tunawakaribisha sana, viongozi wote wa halmashauri hizi za Mkoa wa Morogoro na hususan Morogoro Kusini wafike kwenye Kituo chetu cha Uratibu wa Biashara hii Kituo cha NCMC ili tuweze kuwaongoza na kuwaelekeza namna ya kufanya na hatimaye waweze kuwa sehemu ya washiriki wa biashara hii kubwa ya hewa ya ukaa.

Name

Amosy William Maganga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Sikonge

Primary Question

MHE. JOSEPHINE J. KAPOMA aliuliza: - Je, Serikali ina mkakati gani wa kufikisha elimu kwa wananchi kuhusu Biashara ya Hewa ya Ukaa kwa kuwa ni miongoni mwa biashara kubwa duniani?

Supplementary Question 5

MHE. ENG. AMOSY W. MAGANGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, nami niulize swali. Ni lini sasa wananchi wa Wilaya ya Sikonge nao wataanza kufaidika na biashara hii ya hewa ya ukaa?

Name

Kwagilwa Reuben Nhamanilo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Handeni Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MUUNGANO NA MAZINGIRA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninapenda kujibu swali la Mheshimiwa Amos, Mbunge wa Sikonge ambaye ametaka kufahamu ni lini sasa wananchi wa Sikonge wataanza kunufaika na biashara hii ya hewa ya ukaa?

Mheshimiwa Mwenyekiti, milango iko wazi kuanzia sasa wananchi wa Sikonge kunufaika na biashara hii. Serikali inatambua Sikonge pana misitu mingi kama ambavyo nimejibu swali la nyongeza la Mbunge wa Morogoro Kusini. Tuwaombe sana viongozi ngazi ya halmashauri wafanye mawasiliano na Kituo chetu cha Uratibu wa Biashara hii ya Kaboni ili tuwape miongozo na tuwaongoze katika ushiriki wa biashara hii ya hewa ya ukaa.