Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Ramadhani Hamza Singano
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bumbuli
Primary Question
MHE. RAMADHANI H. SINGANO aliuliza: - Je, Serikali inahakikisha vipi kuwa mikopo ya pato la halmashauri linawafikia vijana?
Supplementary Question 1
MHE. RAMADHANI H. SINGANO: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nipongeze kwa majibu mazuri ya Serikali. Hapa nina maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza, kwa kuwa NIDA ndiyo kitambulisho kikuu cha Kitaifa kwa vijana hawa ili waweze kuwa na sifa za kuomba hiyo mikopo, lakini katika Jimbo langu la Bumbuli maeneo mengi ni tatizo, je, ipi kauli ya Serikali kwa zile mamlaka zinazosimamia hili ili liweze kutekelezwa mara moja, vijana wasikose hii fursa?
Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili. Serikali ina mpango gani madhubuti wa kufuatilia na kuhakikisha kwamba hili jambo linaenda kwa usawa katika maeneo ya majimbo yetu?
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nimpongeze sana Mheshimiwa Eng. Ramadhani Hamza Singano, Mbunge wa Bumbuli kwa namna ambavyo anawakilisha na kuwasemea wananchi wa Jimbo la Bumbuli kwa uthabiti wa hali ya juu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nimhakikishie tu kwamba Serikali baada ya kuweka utaratibu, sheria na kanuni za mikopo ya 10%, eneo la mikopo ya vijana asilimia nne ni eneo ambalo linasimamiwa kwa ukaribu mkubwa kwa sababu Serikali inatambua changamoto ya ajira kwa vijana.
Mhesimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge katika Jimbo la Bumbuli, na katika majimbo yote kote nchini ambako kuna changamoto ya vijana kupata mikopo hii kwa urahisi kwa wakati na kwa uwazi, Serikali itaendelea kuboresha mifumo yake kuendelea kufanya usimamizi na kutoa elimu ili vijana waweze kupata mikopo kiurahisi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili, mkakati wa Serikali ni kuendelea kuboresha, na ndiyo maana tumepitia kanuni zetu za mikopo 2024. Hata hivyo, tunaendelea kufanya tathmini kuona ufanisi wa utoaji wa hii mikopo na tutaendelea kuboresha, lengo likiwa makundi haya ya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu wapate mikopo kwa utaratibu mwepesi zaidi, lakini kwa ufanisi mkubwa zaidi.
Name
Asya Sharif Omar
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. RAMADHANI H. SINGANO aliuliza: - Je, Serikali inahakikisha vipi kuwa mikopo ya pato la halmashauri linawafikia vijana?
Supplementary Question 2
MHE. ASYA SHARIF OMAR: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru kwa kunipa hii nafasi ya kuuliza swali moja la nyongeza. Ninataka kujua, je, katika mikopo hii ya 10%, wanawake wamenufaika vipi, hasa tukizingatia mahitaji yameendelea kuwa makubwa? (Makofi)
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, ninampongeza sana Mheshimiwa Asya, amekuwa msemaji sana wa masuala ya mikopo ya 10%, kuwatetea wanawake kote nchini. Kwa kweli katika hii mikopo ya 10% ambayo inawahusu wanawake, vijana na watu wenye ulemavu, kundi ambalo limenufaika zaidi, lakini limekuwa na muhemko mkubwa wa kupata hii mikopo ni kundi la wanawake.
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mikopo yetu kwa mfano katika kipindi cha Julai, 2024 mpaka Disemba, 2025 Serikali ilipanga kutoa jumla ya mikopo ya shilingi bilioni 253, lakini mpaka Disemba, 2025 imeshatolewa mikopo ya shilingi bilioni 230 sawa na 91%.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, tunaona ufanisi ni mkubwa, vikundi vya wajasiriamali wanawake wameendelea kunufaika, na wapo ambao wame-graduate baada ya kupata mikopo ya 10%, wameweza kujiwekeza zaidi, wamekuwa wafanyabiashara wakubwa na wame-graduate, sasa hawakopi 10%, wanaendelea kukopa kwenye benki na maeneo mengine.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, tutaendelea kusimamia eneo hili kuhakikisha vikundi ambavyo vinakopa vinajenga uwezo wa kiuchumi na ku-graduate, kuhitimu kuendelea mbele wakati tunachukua vikundi vingine ambavyo havina uwezo mzuri wa kiuchumi.
Name
Yannick Ikayo Ndoinyo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ngorongoro
Primary Question
MHE. RAMADHANI H. SINGANO aliuliza: - Je, Serikali inahakikisha vipi kuwa mikopo ya pato la halmashauri linawafikia vijana?
Supplementary Question 3
MHE. YANNICK I. NDOINYO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, nami ninataka kufahamu kutoka kwa Wizara kama ina report iliyoonyesha idadi ya mikopo ambayo wameshaitoa toka wameanza kutoa hii mikopo na ni kiasi gani maisha ya wananchi yamebadilika kwa kutumia hii mikopo? Kama mpo tayari kutuonyesha report kama hiyo.
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, suala hili linahitaji takwimu nami ninaomba nilifanyie kazi, tutampa takwimu Mheshimiwa Mbunge wa Ngorongoro ili tuweze kumpa figure za fedha ambazo zimeshakopeshwa tangu tumeanza na mpaka sasa na marejesho jinsi ambavyo yametolewa.
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Primary Question
MHE. RAMADHANI H. SINGANO aliuliza: - Je, Serikali inahakikisha vipi kuwa mikopo ya pato la halmashauri linawafikia vijana?
Supplementary Question 4
MHE. ATHUMIN O. MAPALILO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Uzoefu unaonyesha kwamba mikopo hii ya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu, mara wanavyoipata inadumu kwa muda mfupi sana, kama miezi mitatu, sita mpaka saba. Baada ya hapo miradi yao inakufa. Sasa ninataka kufahamu, je, Serikali ina mpango gani wa kuhakikisha kwamba miradi hii na mitaji yao inakuwa endelevu? (Makofi)
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, mikopo hii ya 10% ina sura mbili. Sura ya kwanza ni wajasiriamali ambao tayari wanashughuli zao za kiuchumi, wana uzoefu nazo na wanajua marejesho yao yako ndani ya uwezo wa mikopo ambayo wanaichukua.
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika hili kundi tumekuwa hatupati changamoto ya biashara hizo kufa ndani ya muda mfupi, lakini kuna kundi la pili la wale ambao wanaanza kufanya biashara kupitia mikopo ya 10% ambao wamejiunga kama kikundi cha wajasiriamali.
Mheshimiwa Mwenyekiti, hatua ambazo Serikali imechukua, kwanza, tumeanzisha Kamati za mikopo ya 10%, ngazi ya kata, ngazi ya halmashauri na ngazi ya mikoa; Maafisa Maendeleo ya Jamii katika ngazi za kata na halmashauri; watendaji wa kata na tunaelekea kwenye watendaji wa vijiji kuwapa elimu ili kuwawezesha wajasiriamali kupata elimu na mbinu bora za kufanya biashara ili ziwe endelevu na waweze kunufaika na mikopo hii ya 10%.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, tumechukua maoni ya Mheshimiwa Mbunge, tumeendelea kuyafanyia kazi na tutaendelea kuyafanyia kazi ili kuhakikisha hii mikopo inaleta tija kwa makundi yanayotakiwa.