Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Mohamed Mussa Utaly
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Lindi Mjini
Primary Question
MHE. MOHAMED M. UTALY aliuliza: - Je, lini Serikali itakamilisha ujenzi wa Barabara ya Mtange hadi Kineng’ene Kibaoni kwa kiwango cha lami?
Supplementary Question 1
MHE. MOHAMED M. UTALY: Mheshimiwa Spika, ninashukuru sana kwa kunipa fursa hii ya kuuliza swali la nyongeza.
Mheshimiwa Spika, barabara hii ikiwemo pamoja na barabara iendayo katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa pamoja na barabara inayopita katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Lindi zilishaidhinishwa kujengwa katika awamu hii ya mwaka 2025/2026 ambapo mwaka huu wa fedha unaishia mwezi Juni.
Mheshimiwa Spika, hata hivyo, mpaka sasa TAMISEMI haijatoa kibali, ili TARURA iweze kusaini mkataba na mkandarasi. Je, ni lini TAMISEMI itatoa kibali ili TARURA iweze kusaini mkataba na mkandarasi? (Makofi)
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Spika, ninampongeza sana Mheshimiwa Mohamed Mussa Utaly, Mbunge wa Lindi Mjini kwa kazi nzuri anayoifanya kwa ajili ya wananchi wa Lindi Mjini.
Mheshimiwa Spika, ninaomba nimhakikishie tu Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali kwa nia njema imeweka utaratibu, baada ya kutangaza zabuni na kupata wakandarasi kuna utaratibu wa kutoa kibali baada ya kujiridhisha na uwepo wa fedha ili miradi ikianza na wakandarasi wakiwa site kusiwe na mkwamo wa kukosa fedha.
Mheshimiwa Spika, ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, tayari Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI kupitia TARURA imeshapokea maombi ya kupata kibali hicho na sasa wako hatua za mwisho za kutoa kibali hicho ili mkataba huu uanze kutekelezwa kwa ajili ya ujenzi wa barabara hizo. Ahsante sana.
Name
Johannes Lembulung’ Lukumay
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Arumeru-Magharibi
Primary Question
MHE. MOHAMED M. UTALY aliuliza: - Je, lini Serikali itakamilisha ujenzi wa Barabara ya Mtange hadi Kineng’ene Kibaoni kwa kiwango cha lami?
Supplementary Question 2
MHE. JOHANNES L. LUKUMAY: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Tarehe 01 Oktoba, 2025 Mheshimiwa Dkt. Samia alifanya ziara katika Jimbo la Arumeru Magharibi. Katika ziara hiyo aliahidi kujenga Soko la Kisasa la Mji wa Ngaramtoni. Ninapenda kujua Serikali itajenga lini Soko la Kisasa la Mji wa Ngaramtoni?
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Spika, ninaomba nimpongeze sana Mheshimiwa Johannes Lukumay, Mbunge wa Jimbo la Arumeru Magharibi.
Mheshimiwa Spika, ni kweli kwamba Rais, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan alishatoa maelekezo ya ujenzi wa Soko la Kisasa katika Jimbo la Arumeru Magharibi na tayari Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI tumeshaliingiza kwenye mpango wa vipaumbele vya ujenzi wa soko hilo.
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge na wananchi wa Arumeru Magharibi kwamba Serikali hii inaahidi na kutekeleza. Maelekezo na ahadi za Mheshimiwa Rais ni kipaumbele namba moja. Tutahakikisha fedha zinaletwa, tunajenga soko hilo ili kuboresha huduma za biashara kwa wananchi wa Arumeru Magharibi. Ahsante sana.
Name
Asha Salum Motto
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. MOHAMED M. UTALY aliuliza: - Je, lini Serikali itakamilisha ujenzi wa Barabara ya Mtange hadi Kineng’ene Kibaoni kwa kiwango cha lami?
Supplementary Question 3
MHE. ASHA S. MOTTO: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali dogo la nyongeza. Je, ni lini Serikali itakamilisha ujenzi wa barabara kutoka Mnivata – Newala kuelekea Masasi? (Makofi)
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Spika, ninampongeza Mheshimiwa Asha Motto, Mbunge wa Viti Maalum, Mkoa wa Mtwara kwa kufuatilia maendeleo ya barabara na maendeleo mengine katika Mkoa wa Mtwara na kote nchini kwa ujumla.
Mheshimiwa Spika, ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, Serikali imeweka database ya barabara zote ikiwemo Barabara hiyo ya Mtange kwenda Masasi kwa ajili ya utekelezaji wa ujenzi kwa awamu. Tunaendelea kukusanya fedha, kuweka mipango na kutafuta makandarasi kwa hatua na kwa awamu ili tuhakikishe barabara hizo zinajengwa. Ahsante sana.
Name
Josephine Joseph Kapoma
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. MOHAMED M. UTALY aliuliza: - Je, lini Serikali itakamilisha ujenzi wa Barabara ya Mtange hadi Kineng’ene Kibaoni kwa kiwango cha lami?
Supplementary Question 4
MHE. JOSEPHINE J. KAPOMA: Mheshimiwa Spika, ahsante. Morogoro Mjini tuna Barabara ya Tungi ambayo imebakiza kipande kidogo sana, na hii barabara ni kati ya barabara za suluhisho za diversion endapo barabara kubwa ya Msamvu kuelekea Dar es Salaam ina shida. Sasa nilikuwa ninataka kujua mpango wa Serikali wa kumalizia hiki kipande kidogo cha kuunganisha Kihonda – Tungi kuelekea Dar es Salaam.
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Spika, ninampongeza Mheshimiwa Josephine, Mbunge wa Viti Maalum, Mkoa wa Morogoro, lakini nimhakikishie kwamba Serikali inatambua kwamba ziko barabara katika Manispaa ya Morogoro ambazo kwanza zimeharibiwa na mvua nyingi, lakini barabara nyingine ni chakavu ikiwemo barabara ambayo Mheshimiwa Mbunge ameitaja. Lengo na dhamira ya Serikali ni kuendelea kujenga na kuboresha barabara hizo kwa awamu.
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge na wananchi wa Manispaa ya Morogoro kwamba tutaendelea kutenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa barabara hizo. Kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI nitumie fursa hii kuwasisitiza Wakurugenzi wote wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kuweka kipaumbele kwenye fedha za mapato ya ndani kwa mujibu wa maelekezo ya halmashauri ambazo zinakusanya zaidi ya shilingi bilioni 10, ni lazima watenge fedha kwa ajili ya matengenezo na ukarabati wa barabara.
Mheshimiwa Spika, hata halmashauri ambazo zinakusanya chini ya shilingi bilioni 10 kama barabara ni kipaumbele kikubwa katika eneo hilo, ni muhimu watenge fedha kwa ajili ya ukarabati wakati tunasubiri fedha za Serikali Kuu.
Name
Agnesta Lambert Kaiza
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. MOHAMED M. UTALY aliuliza: - Je, lini Serikali itakamilisha ujenzi wa Barabara ya Mtange hadi Kineng’ene Kibaoni kwa kiwango cha lami?
Supplementary Question 5
MHE. AGNESTA L. KAIZA: Mheshimiwa Spika, ninakushukuru kwa kuniona. Mradi wa DMDP II ndani ya Kata ya Vingunguti, Liwiti, Kimanga na Tabata ume-stuck tangu 2023 na sababu kubwa ni Serikali kutokulipa fidia kwa wananchi ambao mradi huo unawapitia, na sasa barabara ni mbovu sana, Naibu Waziri utakubaliana nami. Swali langu kwa Serikali, ni lini italipa fidia na lini ujenzi utaanza kwenye hizi Barabara za DMDP II?
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Ninampongeza sana Mheshimiwa Agnesta Lambert, Mbunge wa Segerea kwa kazi kubwa na nzuri anayoifanya kuwasemea wananchi wa Jimbo la Segerea.
Mheshimiwa Spika, ni kweli kwamba kupitia dhamira nzuri ya Serikali hii ya kuboresha barabara katika Jimbo la Segerea, Mradi wa DMDP II ulianzishwa kwa ajili ya Kata ya Vingunguti, Liwiti, Kimanga na Tabata na eneo lile la barabara lilihitaji fidia kwa wananchi. Serikali ilifanya tathmini na kupata gharama ya awali ya fedha kwa ajili ya kulipa fidia.
Mheshimiwa Spika, kutokana na malalamiko ya baadhi ya wananchi kutoridhishwa na malipo ya fidia, na pia wengine ambao waliendeleza maeneo ambayo walihitaji pia kufanyiwa tathmini, Serikali ililazimika kurejea tena kufanya tathmini mara ya pili.
Mheshimiwa Spika, ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba tayari mwezi wa tatu tumekamilisha uthamini kwa mara ya pili na sasa tuko hatua za mwisho za kulipa fidia, na baada ya kulipa fidia, wakati wowote mapema iwezekanavyo tutaanza ujenzi wa barabara hizi kupitia Mradi wa DMDP II.